Header Ads Widget

MWIGIZAJI BI UBWA WA ZAHANATI YA KIJIJI AFARIKI DUNIA

Mwigizaji mkongwe nchini Tanzania aliyepata umaarufu zaidi kupitia Tamthiliya Zahanati ya Kijiji, Bi Ubwa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa Tamthiliya ya Zahanati ya Kijiji, Abdul Usanga, Bi Ubwa amefariki dunia Aprili 20, 2024.

Hata hivyo, mpaka sasa bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.
Mbali na Zahanati ya Kijiji, Bi Ubwa aliwahi kuwika katika Tamthiliya kama Nuru, Penzini, Simu na nyinginezo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI