Header Ads Widget

RC MAKONDA ALIVYOWASILI AICC KWA AJILI YA KUONGOZA KIKAO CHA WATUMISHI WA MKOA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiwasili kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha, kwa ajili ya kuongoza kikao kazi cha watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa wilaya na Makatibu Yawala wilaya, Wakuu wa Taasisi na wakurugenzi na Menejimenti za Halmashauri za mkoa wa Arusha leo Aprili, 2024.

Katika Kikao hicho, Wakuu wa Taasisi za Umma na Wakurugenzi wa Halmashauri zote saba za mkoa wa Arusha, watawasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ya utawala kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo licha ya uwasilishaji wa taarifa kwenye kikao kazi hicho, Mhe. Makonda anatumia wasaa huo kujitambulisha kwa watumishi na vionhozi wa chama na Serikali wa mkoa wa Arusha ikiwa ni siku ya 12 tangu mkuu huyo wa mkoa kuanza kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Arusha.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI