Header Ads Widget

KAMATI YA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU YATANGAZA ORODHA TEULE, MISWADA 260 YAPOKELEWA

 


Na. Matukio Daima Media, Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya  Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, ametangaza orodha teule ya waliopendekezwa kuwania tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika tarehe 13/4/2026 katika ukumbi wa Superdom Masaki jijini Dar salaam.

Washindi hao wa kila nyanja wamepatikana kutoka kwenye  miswada 260 iliyofanyiwa kazi na majaji wa tuzo hiyo  ikihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na washiriki wapya kutoka nje ya nchi. 

Akizungumza na vyombo vya habari Aprili 8, 2026 jijini Dodoma, Prof. Mlama amesisitiza kuwa mwitikio wa mwaka huu umekuwa mkubwa na ni ishara ya hamasa ya waandishi kushiriki katika kukuza fasihi na uandishi bunifu.  

Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama akitangaza orodha teule 

Ameongeza kuwa Washindi wa kila nyanja watatangazwa rasmi Aprili 13, 2026 na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vyeti.

Ameendelea kusema kuwa, mshindi wa kwanza, muswada wake utachapishwa na Serikali itanunua nakala kwa ajili ya shule na maktaba za taifa ili kuendeleza fasihi na kuhamasisha uandishi bunifu nchini.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI