Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH BILIONI 3.6 WILAYA YA SAME


 Mkuu wa wilaya Same Kasilda Mgeni kushoto,akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Kwa Mkuu wa wilaya ya Mwanga,Mkoani Kilimanjaro .

Na Matukio Daima App,Same

Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 umepokelewa wilayani Same , baada ya kumaliza mbio zake kwenye wilaya ya Mwanga makabidhiano yamefanyika viwanja vya shule ya Msingi Njoro halmashauri ya Wilaya ya Same.


Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amepokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya akisema ukiwa wilayani humo  utakimbizwa umbali wa KM 138.4 kutembelea, kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua jumla ya  miradi Nane (8) yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni  3.6.


Wilaya ya Same inakua wilaya ya Saba kwenye mkoanwa Kilimanjaro na ndio itahitimisha mbio ni hizo kimkoa kwa mwaka huu 2024, kisha kukabidhi mkoa jirani wa Tanga hapo kesho Aprili 9,mwaka huu 2024.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI