ZAIDI ya kaya 1000 zipo hatarini kukumbwa na magonjwa ya tumbo, kipindupindu, kichocho na magonjwa mengine ya mlipuko kutokana na Maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Nachingwea.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo, wananchi walisema kuwa asilimia kubwa ya vyoo vimebomoka hivyo hawana phala pa kujisaidia na maji wanakunywa ya visimani na kwenye mabonde jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Akitolea ufafanuzi mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa serikali imejipanga kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yasitokee ndio maana sasa wanagawa vidonge vya kutibu maji ili wananchi wasidhurike.
Kwa upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Joseph Massiah alisema kuwa wanagawa bure vidonge vya kutibu maji zaidi ya elfu 64,000 kwa wananchi wote walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha.
Massiah alikiri vyoo vingi vimebomoka hivyo wananchi wanatakiwa kuishi kwa tahadhari kubwa ya kulinda afya zao.
0 Comments