Header Ads Widget

MTEMVU AONGOZA CCM MKOA WA DAR KUTOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI








Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Abas Mtemvu ameongoza viongozi na Wana CCM mkoa wa Dar es salaam kukabidhi Msaada wa mahitaji ya chakula na vifaa kwa Waathirika wa mafuriko katika kata 12 za wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.


Akizungumza wakati wa kukabithi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya milioni 22 kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele huko katika viwanja vya shule ya msingi Umwe Ikwiriri amesema amekuja kutekeleza ahadi yake aliyotoa wiki iliyopita wakati alipokuja Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Abdulamani Kinana.


Alisema kuleta msaada huo ni kutekeleza agizo la Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM aliloagiza siku hiyo alipofika kutembelea na kuzungumza na waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya ya Rufiji kwani baada ya ujio ule Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Dar es salaam akapokea simu za Wadau mbalimbali wakitaka kuchangia kutoa msaada huo kwa Waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya ya Rufiji.


Alisema asili ya Dar es salaam ni mkoa wa Pwani na huwezi kuitoa Dar es salaam katika mkoa huo wa Pwani hivyo wamesema lazima waje kuleta msaada huo iliwashiriki kutoa walichonacho na wao kwa kuleta msaada huo kwa ndugu zao.


Mtemvu alisema aliporudi walikutana na kuunda timu yao iliyofanikisha kupatikana kwa misaada hiyo chakula na vifaa umetolewa na wanaCCM kutoka mkoa wa Dar es salaam na Wadau wake akiwemo Amo Foundation, 


Awali Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alishukuru kwa msaada huo kutoka kwa Wana CCM, Wananchi na Wadau wa mkoa wa Dar es salaam na kusema zoezi la kuhamisha Wananchi mashambani bado litaendelea ilikupisha mafuriko hayo.


Pia Meja Gowele alisema tayari uongozi wa Wilaya umetenga viwanja zaidi ya mia 6 kwaajili ya Wananchi waliokumbwa na mafuliko hayo maeneo yao na kusema eneo hilo ni salama halitakuja kufikiwa na mafuriko.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Rogart Mbowe alisema Mwenyekiti wa CCM huyo wa mkoa wa Dar es salaam baada ya kutoka Rufiji katika ziara ya Mheshimiwa Kinana hakulala akawaagiza wenyeviti wa CCM Wilaya za mkoa wa Dar es salaam watafute misaada hiyo ilikuja kuleta kwa ndugu zao wa Wilaya ya Rufiji walioathiriwa na mafuriko hao.


Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya AMO foundation. Amina saidi ambaye amehusika kuchangia misaada hiyo zaidi ya tani kumi za unga wa sembe ambapo amezitaka Taasisi na mashirika yasiyoya kiserikali kupeleka misaada yao ya hali na Mali kwa waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya ya Rufiji.


Mwenyekiti wa jumuhia ya Wazazi mkoa wa Dar es salaam Hadija Ally Saidi alitaka vyakula zaidi ya tani 13 walivyoleta kuwa ni mchele , maharage, unga wa sembe, makatoni ya maji ya kunywa, magodoro 100 na kusema hiyo yote ni matokeo ya Siasa safi ya CCM kuanzia ngazi ya Taifa inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, CCM mkoa wa Dar es salaam na mahusiano na Wadau wake.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji Kaswakala Mbonde alishukuru kwa msaada huo uliotolewa na CCM mkoa wa Dar es salaam na kuelezea kuwa hali ya mafuriko wilayani humo yanahistoria ya zaidi ya mia 50 hivyo amewataka Watanzania kutokubali kupotoshwa kuhusu wanasema mafuriko hayo ni athari za Bwawa la kuzalisha Umeme Mwalimu Julias Nyerere.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI