NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameshiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Mwika kata ya Mwika Kaskazini, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 120.4 na kukagua miradi saba ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi yenye thamani ya Bilioni 2.3 na badae kukesha stendi ya mabasi kata ya Njiapanda.
Unumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ni "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Mwisho.
0 Comments