NA JOSEA SINKALA, MBEYA.
Jamii imeombwa kuendelea kusaidia waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea katika Kata ya Itezi Uyole jijini Mbeya kwani mpaka sasa wananchi wengi bado wanaishi kambini katika shule ya msingi Tambukareli Uyole.
Rai hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Itezi Mhe. Sambwee Shitambala wakati akipokea msaada wa mafuta lita miamoja kutoka kwa Shule ya msingi Mary's iliyopo Itezi viwanja vipya.
Diwani Shitambala ameishukuru shule ya Mary's ambayo ni jirani na sehemu iliyokumbwa na kadhia ya maafa ya maporomoko ya tope lakini haijaguswa moja kwa moja na maafa hayo akisema uongozi wa shule hiyo umeguswa kuwasaidia majirani ambao wamekumbwa na kadhia hiyo na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuungana na Serikali kusaidia waathirika hao.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo wa mafuta ya kupikia, Mkurugenzi wa Shule ya Mary's amesema wameguswa baada ya kuona wananchi wengi ambao ni jirani na shule yao wkaikumbwa na maafa hayo.
Amesema wanamshukuru Mungu kw shule yao kunusurika lakini makazi ya wananchi ambao ni majirani zao wameathirika kwa makazi na mazao yao kuharibika vibaya na kueleza matumaini kuwa kwa Serikali.
Wananchi waliokumbwa na maafa hayo wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali pamoja na wadau na mtu mmoja mmoja wanaofika kwa ajili ya kuwafariji wakiwemo shule ya msingi Mary's.
Rosemary Pesambili ni mdhibiti ubora Mkuu wa shule Jiji la Mbeya pamoja na kufika na ujumbe wake shuleni hapo kutoa msaada wao pia amesema shule ya Mary's haijaathirika isipokuwa kwa sasa shule tatu zimesitisha masomo kwa muda na shule moja ya Generation ndio imeathirika kabisa
0 Comments