Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
WALIMU wa Shule za Msingi nchini wametakiwa kutowarudisha nyumbani wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia michango mbalimbali na badala yake waachwe kuendelea na masomo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Aprili 5,2024 wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathmini ya Sekta ya elimu kwa mwaka 2023/2024 uliohusisha wadau mbalimbali wa elimu kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo na kuleta mageuzi katika elimu.
Amesema hakuna utaratibu wa Serikali wa kumrudisha mwanafunzi nyumbani kwa kukosa michango kwa kuwa dhana ya elimu bila ada inaelekeza mtoto asinyimwe kwenda shule kwa kukosa michango na kufafanua kuwa hakuna adhabu yoyote itakayofanya mtoto akose masomo.
Waziri Mkenda amesema licha ya changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo,Walimu wanapaswa kuheshimiwa ili kuwafanya wanafunzi kuwa bora huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuleta mageuzi kuanzia ngazi ya chini hadi vyuo vikuu.
Kwa upande wake Kamishina wa Elimu Dkt Lyabwene Mtahabwa amesema katika kaikao chicho kilichowachukua muda wa siku tatu wamejadili na kuadhimia kwenda kuyafanyia kazi maeneo 10 ambayo yatakwenda kileta ufanisi katika Elimu.
Amesema jambo la kwanza ni kuboresha vikao na Mikutano ya pamoja ya tathimini katika sekta ya elimu ili kileta matokeo chanya.
Ameeleza , chakula na lishe mashuleni ambapo wadau hao wa sekta ya elimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wameadhimia ikiwezekana sheria itungwe kwa wazazi wachangie masuala mazima ya elimu pale inapobidi kwani bila afya akili hakuna.
Maadhimio mengine ni kwenye eneo la mitaala ambapo wametaka kupelekwe Sera za mitaala ili kulahisisha wadau walimu katika utendaji kazi
Jambo jingine amesema waneona elimu ya juu ihakisi mabadiliko yote yalifanyika kuanzia elimu ya ngazi ya chini, bila kusahau kuimalisha ushirikiano kati ya wizara na wadau Mbalimbali wanaotoa elimu hapa nchini na nje ya nchi
Aidha amesema eneo lingine ni kuhakikisha wanajikita katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi bila kusahau hisabati pia na kutafuta mbinu na mikakati ili kupata rasilimali kuendesha elimu
Hata hivyo amesema eneo lingine ni kwenye elimu ya watu wazima imesahaulika mfumo wake, lakini pia uchangishwaji wa elimu kwa jamii na sio lazima iwe ni fedha pekee bila kusahau serikali na wadau kupeana mafunzo Mbalimbali juu ya elimu.
0 Comments