Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO VUNJO

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MWENGE wa Uhuru mwaka 2024 umezindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 924 Jimbo la Vunjo, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. 


Miradi ilyozinduliwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Darajani iliyopo kata ya Njiapanda iliyogharimu shilingi milioni 348 na mradi mkubwa wa uboreshaji huduma ya maji kijiji cha Yamu Makaa kata ya Kirua Vunjo Kusini unaogharimu shilingi milioni 576.



Pia Mwenge wa Uhuru ulizindua mradi wa utunzaji Mazingira kata ya Marangu Mashariki na klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Pumuani kata ya Kirua Vunjo Kusini. Katika miradi yote hii miti ipatayo 1,200 imepandwa ili kutunza mazingira. 


Katika kutekeleza kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu msafara wa Mwenge wa Uhuru ulishiriki pia shughuli za Upandaji miti ili kutunza mazingira.



Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Stephen Kimei ameshiriki kikamilifu mbio za Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la uwakilishi. 


Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea leo upande wa Jimbo la Moshi Vijijini na baadae jioni utakesha katika viwanja vya stendi ya mabasi kata ya Njiapanda.



Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu."

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI