Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WAKATI Tanzania ikiadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kumekuwepo na ongezeko la Majaji wa Rufani ambapo Ongezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani limeenda sambamba na uanzishwaji wa Masjala ndogo ya Mahakama ya Rufani nchini.
Hayo yamesema leo jijini hapa na Mtendaji mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akieleza mafanikio ya miaka 60 ya muugano wa Tanzania bara na Zanzibar ameeleza wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani Machi 2021 kulikuwa na Majaji wa Rufani 16 na katika uongozi wake hadi kufikia 03 Septemba 2023 idadi ya Majaji wa Rufani imeongezeka na kufikia 35 ikiwa ni zaidi asilimia 100.
Amesema ngezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa linawezesha majopo 11 ya majaji watatu, majopo saba ya Majaji watano na majopo Matano ya Majaji saba kuendesha vikao vya Mahakama ya Rufani kwa wakati mmoja.
Pia ameeleza idadi ya Vituo vya kusikilizia mashauri ya Mahakama ya Rufani imeongezeka na kutoka 16 wakati wa Dkt. Samia akiingia madarakani na kufikia vituo 18 mpaka sasa.
"Vituo vya usikilizaji wa Mashauri ya Mahakama ya Rufani viko katika Masjala za Mahakama Kuu za Arusha, Dar es Salaam, Bukoba, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Moshi, Musoma, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songea, Sumbawanga, Tabora, Tanga na Zanzibar, " Prof Elisante.
Na kuongeza "Kumekuwepo na faida zilizotokana na kuongezeka kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ikiwa ni pamoja na kupunguza mrundikano wa mashauri, kusogeza huduma karibu zaidi na Wananchi katika Masjala zote za Mahakama Kuu, Mashauri kusajiliwa na kuamuriwa kwa wakati na kupungua mzigo kwa majopo yaliyokuwepo, " Amesema Mtendaji huyo.
Aidha amesema Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Pemba, ambao utaanza hivi karibuni ni miongoni mwa mafanikio yanayolenga kusongeza huduma za utopaji haki karibu na wananchi.
Amebainisha kuwa,Uwepo wa Kituo hicho utaiwezesha Mahakama ya Rufani kuwa na Masjala yake ndogo, hivyo kuongeza idadi ya Vikao vya Mahakama kwa upande wa Zanzibar.
Mwisho
[4/5, 9:31 PM] HAMIDA RAMADHAN MDTV DODOMA: MARUFUKU KUWARUDISHA WANAFUNZI WALIOSHINDWA KUCHANGIA MICHANGO
Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
WALIMU wa Shule za Msingi nchini wametakiwa kutowarudisha nyumbani wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia michango mbalimbali na badala yake waachwe kuendelea na masomo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Aprili 5,2024 wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathmini ya Sekta ya elimu kwa mwaka 2023/2024 uliohusisha wadau mbalimbali wa elimu kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo na kuleta mageuzi katika elimu.
Amesema hakuna utaratibu wa Serikali wa kumrudisha mwanafunzi nyumbani kwa kukosa michango kwa kuwa dhana ya elimu bila ada inaelekeza mtoto asinyimwe kwenda shule kwa kukosa michango na kufafanua kuwa hakuna adhabu yoyote itakayofanya mtoto akose masomo.
Waziri Mkenda amesema licha ya changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo,Walimu wanapaswa kuheshimiwa ili kuwafanya wanafunzi kuwa bora huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuleta mageuzi kuanzia ngazi ya chini hadi vyuo vikuu.
Kwa upande wake Kamishina wa Elimu Dkt Lyabwene Mtahabwa amesema katika kaikao chicho kilichowachukua muda wa siku tatu wamejadili na kuadhimia kwenda kuyafanyia kazi maeneo 10 ambayo yatakwenda kileta ufanisi katika Elimu.
Amesema jambo la kwanza ni kuboresha vikao na Mikutano ya pamoja ya tathimini katika sekta ya elimu ili kileta matokeo chanya.
Ameeleza , chakula na lishe mashuleni ambapo wadau hao wa sekta ya elimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wameadhimia ikiwezekana sheria itungwe kwa wazazi wachangie masuala mazima ya elimu pale inapobidi kwani bila afya akili hakuna.
Maadhimio mengine ni kwenye eneo la mitaala ambapo wametaka kupelekwe Sera za mitaala ili kulahisisha wadau walimu katika utendaji kazi
Jambo jingine amesema waneona elimu ya juu ihakisi mabadiliko yote yalifanyika kuanzia elimu ya ngazi ya chini, bila kusahau kuimalisha ushirikiano kati ya wizara na wadau Mbalimbali wanaotoa elimu hapa nchini na nje ya nchi
Aidha amesema eneo lingine ni kuhakikisha wanajikita katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi bila kusahau hisabati pia na kutafuta mbinu na mikakati ili kupata rasilimali kuendesha elimu
Hata hivyo amesema eneo lingine ni kwenye elimu ya watu wazima imesahaulika mfumo wake, lakini pia uchangishwaji wa elimu kwa jamii na sio lazima iwe ni fedha pekee bila kusahau serikali na wadau kupeana mafunzo Mbalimbali juu ya elimu.
0 Comments