Header Ads Widget

ZAIDI YA MITI 1.9M KUPANDWA K'NJARO

Na Gift Mongi, MATUKIODAIMA APP,MOSHI

Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kutunza uoto wa asili uliopo katika nyanda za juu mkoani Kilimanjaro miti 85,794 imepandwa katika maeneo hayo.


Miti hiyo imepandwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya shule,vyanzo vya maji,barabara na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.


Mkurugenzi wa shirika la Floresta Tanzania Richard Mhina amesema kuwa katika robo mbili za mwaka miti hiyo imepandwa katika awamu mbili ambazo ni robo mbili za mwaka.


Anaeleza kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka miti 136,404 ilipandwa huku robo ya pili ambayo ilikuwa na mvua nyingi miti 69,390 ilipandwa na lengo likiwa ni kufikia idadi ya miti 1,902,630 Kwa mwaka.

Anasema kuwa shirika hilo la Floresta Tanzania limekuwa likifanya kazi na jamii,serikali,na wadau wengine wa mazingira Kwa muda sasa.


Kwa mujibu wa Mhina ni kuwa wao wamekuwa wakiwawezesha jamii kupata miche na kuwa jukumu lao ni kupata mbegu na viriba kwa ajili ya vitalu huku jamii ikijengewa dhana ya utayari.


Anafafanua kuwa mbali na jitihada hizo zote ambazo wanazifanya kama shirika bado ipo changamoto kubwa ya uharibifu wa miti yenyewe jambo linalofanya kushindwa kupiga hatua


'Niziombe mamlaka zenye jukumu la kusimamia mazingira wafanye hivyo wakiwemo viongozi wa vijiji na vitongoji ambao ndio wapo karibu zaidi na jamii'anaeleza


Anasema wote kwa pamoja wakiungana katika kukemea na kupambana na vitendo hivyo watakuwa wamefanikiwa Kwa kiwango kikubwa kutengwneza mazingira rafiki na kuyafanya endelevu.


Mdau wa mazingira Dkt Glorious Shoo amesema ipo haja kuwepo na taasisi ambazo zitakuwa zinatoa motisha kwa mtu au kikundi ambacho kitakuwa kimetunza mtu kwa zaidi ya mwaka.


Anasema kama ambavyo jitihada za kupanda miti zinavyofanyika basi hivyohivyo ziwepo jitihada za kuhakikisha miti hiyo inatunzwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI