Na Mwandishi wetu,Matukio daimaapp
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Mtwara leo imepokea mitambo miwili ya kupakua na kupakia mizigo yenye uwezo wa kubeba zaidi ya tani 160 ikiwa ni utelekezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu wakati wa ziara yake Mkoani Mtwara aliyoifanya Septemba mwaka jana.
Akizungumzia ujio wa Mitambo hio Bandarini leo Machi 12, 2024, kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania Plasduce Mbossa, Nicodemus Mushi amesema kuwa mitambo hiyo imekuja kufanya maboresho makubwa katika bandari hiyo.
Amesema kuwa kwa sasa Bandari hiyo imekuwa na uwezo wa kufanyakazi katika kipindi chote cha mwaka.
“Unajua Mhe. Rais alitaka kufanyike uwekezaji wa Vifaa ambavyo awali bandari hiyo ilikuwa ikihudumia shehena ya tani laki nne kwa mwaka baada ya uwekezaji na maboresho makubwa bandari hiyo imeongeza kasi ya utendaji ambapo kwa sasa inahudumia shehena yenye uzito wa tani milioni moja” amesema Mushi
Naye Mhandisi Humphrey Kiwia amesema kuwa mitambo hiyo imetokea katika Bandari ya Dar es salaam yenye uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo tani 100 na Tanga shehena ya tani 63 na kufanya jumla iwe tani 163.
Kwaniaba ya Meneja wa Bandari Mtwara Dunkan Kazibure amesema ukarabati mkubwa wa bandari umefanyika kwa kiasi kikubwa ambapo zaidi ya shilingi bilioni 157 zilitumika.
Amesema kuwa maboresho hayo yamefanyika katika kwenye gati mpya ambapo uwepo wa vifaa vyenye uwezo mkubwa kufika vinaongeza ufanisi zaidi.
“Bandari yetu imefanyiwa ukarabati mkubwa hivyo uwepo wa vifaa vikubwa utaongeza uwajibikaji na uboreshaji wa huduma ambapo tunaamini kuwa tutapata mizigo zaidi ya kupakia na kupakua katika bandari yetu”
“Kwasasa tuna matarajio makubwa ya kuongeza uzalishaji na kupata mizigo mingi zaidi kuweza kusafirishwa kupitia bandari yetu ambapo tunatarajia kuongeza hadi kufikia tani milioni moja na laki mbili”
“Zamani tulikuwa tunaitumia hii bandari wakati wa msimu wa msimu wa korosho tu na ukiisha tunakuwa hatuna kazi lakini sasa mwaka mzima tunaitumia ambapo imeongeza mapato, ajira na kufanya mji uchnagamke kwa kiasi kikubwa sasa uboreshaji huu unaleta faida nyingi zaidi” amesema Kazibure
0 Comments