Na Mwandishi wetu Matukio daimaapp. Bagamoyo
Zaidi ya watalii 35,436 wamefanya utalii katika halmashauri ya wilaya ya bagamoyo ambapo wameingiza zaiidi ya shilingi 78,302,000.
Akitoa taarifa ya kituo hicho Mhifadhi wa Malikale Rossalia Burreta amesema kuwa Magofu ya Kaole Madiwani wa Halmashauri ya Mji Nanyamba watembelea utalii Bagamoyo wakiwa katika ziara ya siku moja ambapo wametembelea vituo vya malikale ambapo watalii wameongezeka.
Amesema kuwa kuanzia karne ya tisa Washirazi walianzisha makazi yao ya kudumu katika maeneo ya Pwani wakianzia Somalia(Mogadushi), Lamu(Mombasa), Kaole Kilwa, Kisiwani, Songomnara na Kunduchi (Dar es salaam).
“Kituo cha Magofu kaole kinahifadhi masalia ya kihistoria(karne ya 13 na 15) ya msikiti, makaburi na msingi wa nyumba pamoja na makumbusho yaliyoanzishwa kuhifadhi malikale zinazokusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya Pwani”
“Unajua umaarufu wa mjimkongwe wa Bagamoyo unatokana na biashara ya utumwa na pembe za ndovu hasa katika karne ya 19 na kupelekea kwa jina la bagamoyo kuanzishwa ambapo paliitwa Pwani ya juu ila watumwa walipo wasili waliita bwagamoyo ikimaanisha pumzisha moyo wako kwani walikata tamaa ya uwezekano wa kurejea makwao, kutokana na wageni kushindwa kutamka neno Bwagamoyo ikitamkwa” amesema Burreta
Nae Salum Omary Tino Diwani Mnima amesema kuwa amefurahi kuona utalii ukiwa umepewa nafasi kubwa zaidi hivyo kuongeza mapato katika halmashauri hiyo.
“Sisi tumekuja kaole kuona maeneo ya historia ni eneo la kitalii ambalo kiukweli tunaona eneo linalovutia kwa utalii na eneo ambalo ni moja kati ya maeneo ambayo ya naingiza mapato katika Halmashauri hii ya wilaya ya Bagamoyo tunakitu cha kujifunza” amesema Tino
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba Kapeme Jamal amesema kuwa safari hiyo ni ya kujifunza imewapa nafasi za kufanya utalii katika maeneo ya mali kali.
0 Comments