Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI WAZIDI KUIMIZA AMANI KUELEKEA OKTOBA 29

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesisitiza umuhimu wa kutanguliza amani na maslahi ya wengi mbele katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu na hata baada ya zoezi hilo kukamilika, akisisitiza umuhimu wa kutokumbatia jambo baya hasa kwa kutazama mifano dhahiri ya yale yanayoendelea katika Mataifa ya jirani na yale yenye ukosefu wa amani.

Mufti Zubeir amesisitiza hayo leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 wakati wa Kongamano na Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali Jijini Dar Es Salaam akirejea mfano wa hadithi za Haruni katika enzi za Musa katika Maandiko ya dini na namna ambavyo Mungu alimuangamiza Mtu huyo mara baada ya kukaidi maagizo na maonyo ya watu wake wakaribu waliokuwa wakimtaka kutenda wema na kuacha kuichafua nchi yake kutokana na tabia zake.


"Mwenyenzi Mungu anasema ana wivu zaidi kuliko sisi, wivu wa Mungu hataki kuona kiumbe chake kinadhulumiwa, watu wanaharibu amani ama watu wanaharibu nchi. Ipo ibada ya Hijja kwenye nguzo za uislamu, kila mmoja huwa anatamani kwenda na hata mtu akifikia uwezo wa kuweza kwenda kule anapoenda kukiwa hakuna amani anaambiwa  asiende licha ya kuwa na nauli na kila kitu na hii ni kwasababu amani ni kila kitu." Amesema Mufti na Sheikh Mkuu huyo


Mufti katika hotuba yake amerejea pia maandiko ya Mwenyenzi Mungu na kusisitiza kuwa hapendi watu waharibifu na wenye kutanguliza maslahi yao, akibainisha umuhimu wa amani na namna ambavyo kila mmoja anawajibika kuilinda na kuitetea kwa mustakabali wa wengi kama ilivyokuwa amri ya Mwenyenzi Mungu katika kuitunza dunia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI