Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amemaliza mgogoro ulioibuka kufuatia tetesi za kuhamishwa kwa makao makuu ya Tarafa ya Kwaruhombo. Akizungumza na Wananchi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ndugu Ridhiwani Kikwete alieleza kusikitishwa kwake na taharuki hiyo kwa kuwa sio jambo walilotaraji lingefikia hapo hasa ukizingatia kuwa wako viongozi wengi katika kata ambao wana uwezo wa kumaliza changamoto za namna hiyo.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza , Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa makao makuu hayatohama kwa kuwa sababu za ofisi hiyo kuwepo hapo hazijabadilika hivyo Ujenzi wa ofisi uanze mara moja.
Makandarasi wa ujenzi amekabidhiwa eneo na ujenzi unataraji kuanza mara moja. Fedha za ujenzi zimekwishatolewa
0 Comments