Na Hamida Ramadhani, Matukio Daima App Dodoma
WANAWAKE wametakiwa kuwa na nguvu moja ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya waasisi wanawake akiwemo Bibi Titi Mohamed ambao kwa namna moja au nyingine walipigania nguvu na umoja wa wanawake
Hayo yameelezwa jana Jijini hapa kwenye tukio la usiku wa wananwake, uchumi, na familia Kamishna Msaidizi wa Idara ya maendeleo ya Sekta ya fedha Wizara ya fedha Janeth Lewis Hiza ambapo amesema hata kama huna mtoto wewe ni mama unaweza kuwa umuhimu kwa wanawake wengine na ukawa mlezi kwa watoto wengine
Amesema kunamsemo inaosema wanawake hawapendani msemo huo ameotaka kutotumika tena na badala yake uzoeleke msemo usemao wanawake ni keshi kubwa.
Aidha amesema ili kujenga uchumi wa mwanamke ni lazima mwanamke akubali kushaurika,kujifunza kwawenzake waliofanikiwa
" Wanawake Tunachangamoto ya matumizi mabaya ya muda mtu anakaa massage zaidi ya masaa 3 anachezea simu bila faida lazima ujue unafaidikaje na simu tangu umeitumia Kuwa mama inahitaji ujasiri lazima uwe na maamuzi magumu ," Amesema .
Akizungumza kuhusu uchaguzi amewataka wanawake kujitokeze kushiriki kikamilifu katika nafasi za mitaa ili kupata nafasi ya kujipambania kumaliza matatizo yao
Kuhusu maadili amewataka wanawake kuwalea watoto na vijana kwa maadili kwani kuna shida kubwa ya mmomonyoko wa maadili hivyo kwa ukaribu wa kuzungumza Mara kwa Mara na watoto wanaweza kuwa katika maadili yanayotakiwa.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Women (DIWO) Shamsa Danga amewataka wanawake Kuachana na fikra potofu zozote zinazokwamisha maendeleo ya kiuchumi
"Badala yake Kuweni na fikra bunifu kwenye jamii mpya Jamboree litakalowafanya kuepukana na changamoto zilizopo kwenye jamii," Amesema Mkurugenzi huyo Shamsa
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt, Deograsia Nduguru amezungumzia ukombozi wa mwanamke kifikra ambapo ameeleza kuwa mwanamke ana nchango mkubwa na kuendeleza amani mwanamke anapaswa kuhishughulisha katika uzalishaji na afya
Familia inaweza kukua kiuchumi ikiwa msingi wa uzalishaji utapewa kipaumbele kwa kuzingatia malezi na elimu kwa watoto.
"Tu natakiwa kupewa hadhi tunayostahili, mwanamke bunifu huweza kujipambanua na kujiweka katika nafasi , mkono uleao mwana ndio uleao taifa," Amesema
Meakilishi kutoka TGNP Mtandao Lilian Liundi Mkurugenzi Mtendaji ameitaka serikali kuwekwa Bajeti yenye mtizamo wa kijinsia bajeti ambayo itakuwa ya uchambuzi wa hali halisi ya makundi tofauti katika jamii kwa kuzingatia jinsi,rika kulingana na mahitaji
Amesema Bajeti nyingi zinatengenezwa lakini hazina jicho lakina la uchambuzi wa vigezo vya kijinsia ambapo Mahitaji ya watu wenye ulemavu hayaendani na ya watu wa kawaida Wajawazito pia lishe Yao ni tofauti, anayenyonyesha pia lishe inahitaji bajeti lakin Mara ngapi familia wanajadili bajeti
"Hatua za bajeti ya kijinsia kuwepo na vipaumbele vya mahitaji kulingana na kipato na baadae utekelezaji kwa kuzingatia matokeo tarajiwa ili kujua mapungufu na maboresho zaidi , " Amesema
Na kuongeza "Ni muhimu kuzungumzia maendeleo kwa kuhusisha na bajeti ya ngazi ya familia Kipato cha familia kikoje nani anachangia kipato hicho Kuna kipato huduma ambacho hufanywa na mwanamke ambapo Mara nyingi watu wahakihesabu,"Amesema
Hata hivyo Kuelekea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,shirika la Dira Women (DIWO) limewakutanisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma katika usiku wa mwanamke, uchumi na familia ili kuwaleta pamoja
Mwisho
0 Comments