NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANANCHI wa vijiji vya Boro na Kirima katika kata ya Kibosho Kirima jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro wanaenda kuondoka na changamoto ya daraja la Kitarakyamburu baada ya serikali kuanza kulijenga.
Shughuli ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo umeshuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi pamoja na mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ambaye ni Meneja wa Tarura mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Nicholaus Francis.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa, dini, Serikali, mjenzi wa daraja hilo Kuringe Construction, Msimamizi wa Mradi huo
Mhandisi Mchanga kutoka TARURA wilaya na wananchi kutoka vijiji jirani.
Katika uzinduzi huo, Mhandisi Francis aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa ubunifu wao na kuwaambia kwamba, ofisi yake ya TARURA itatoa ushirikiano katika hatua zote muhimu za ujenzi huo pamoja na kuboresha barabara inayofika hapo darajani.
Mhnadisi Francis pia alishriki katika zoezi la kupanda mti katika eneo hilo.
Mbunge aliwashukuru wadau wote waliochangia, na ameomba wadau waendelee kuchangia kwani bado kiasi cha shilingi milioni 74 zinahitajika.
Amewaomba wazawa wa maeneo hayo washiriki kikamilifu kuchangia raslimali fedha na nguvu kazi katika ujenzi huo.
Mwisho..
0 Comments