Header Ads Widget

WANANCHI WATOLEWA HOFU HUDUMA HOSPITAL ZA RUFAA ZA MIKOA

 




Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma


WANANCHI wamehakikishiwa kuwa Hosptali za Rufaa za Mikoa zimejipanga kuwahudumia wagonjwa wote kwa ubora tena kwa masaa 24 ikiwa ni pamoja na wale wanaotumia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), fedha taslimu pamoja na wale wa msamaha. 



Akizungumza jijini Dodoma Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest ambaye pia ni Mwenyekiti  Mfawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Tanzania Bara amesema kuwa kitita cha kutolea huduma hasa kwa wagonjwa wanaotumia bima ya NHIF, kimeboreshwa ambapo dawa nyingi zimeingizwa ambazo hazikuwepo awali


Dkt. Ibenzi amefafanua kuwa Rais Dk. Samia  Suluhu Hassan amefanya uwekezaji  katika kuongeza wataalamu wa afya, vifaa tiba, dawa pamoja na vitendanishi katika Hospitali za mikoa ambazo zimeimarika kwa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.


Amesema jana walikuwa na kikao cha waganga wafawidhi kutoka mikoa 28 nchini ambapo walikubaliana kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi wagonjwa hao watakapomalizika tofauti na awali walivyokuwa wakitoka kazini saa tisa na nusu jioni.


Mganga Mfawidhi huyo ameeleza kuwa lengo ni kuwahudumia wangonjwa wao kwa wakati bila kusababisha ukosefu wa huduma katika maeneo yao ya kazi.


Aidha wameishukuru Wizara ya afya kwa kuendelea kuzisimamia hospitali zote za Rufaa za mikoa kuziwezesha kwa kuleta wataalam wa kutosha


" Hivi karibuni imeajiri wataalam lengo kubwa ni kuziba mapengo yaliyowepo, serikali ya awamu ya sita imewekeza kwenye sekta ya afya na wizara nayo imepanga mipango yake ili kuwezeaha kupata wataalam," ameeleza.


Na kuongeza "Tunamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya katika nchi na kwamba wapo katika mwendelezo wa uboreshaji wa huduma za afya hapa nchini na  wanajua uwekezaji makubwa katika sekta ya afya uliofanywa na Rais huyo wa awamu ya sita.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI