Header Ads Widget

JAMII YAELIMISHWA JUU YA MADHARA YA KUTUMIA VITI MWENDO VISIVYO SAHIHI

 .








NA  NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Jamii imetakiwa  kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaohitaji viti mwendo(wheel chair)wanapata visaidizi sahihi ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na kutumia vitimwendo visivyo sahihi kama vile kupinda mgongo pamoja na vidonda mgandamizo.



Rai hiyo imetolewa na wadau mbalimbali jana Machi 1,2024 katika maadhimisho ya siku ya viti mwendo Duniani yaliyofanywa na Taasisi ya KyaroAssistive Tech kwa kushirikiana na Tai Tanzania ikiwa ni sehemu ya kusherehekea nguvu ya kiti mwendo namna ambavyo inaweza kutoa fursa kwa mtu mwenye ulemavu kufanya mambo yanayoweza kubadilisha maisha yake kwa ukamilifu.


Akiongea wakati wa maadhisho hayo Mkurugenzi wa Kyaro Assistive Tech Colman Ndetembea, taasisi inayojihushisha na uzalishaji na usambazaji wa viti mwendo na vifaa saidizi mbalimbali, alisema kuwa wamekusanyika na wadau mbalimbali ili kuweza kuelimisha jamii juu ya kiti mwendo sahihi na umuhimu wake pamoja na hatari inayoweza kutokea endapo mtu atapata kiti mwendo kisicho sahihi.



Ndetembea alieleza kuwa wameamua kushiriki na dunia nzima kuadhimisha siku hiyo baada ya kuona watu wengi wanatumia viti mwendo visivyo sahihi aidha kwa kupewa misaada au kwa kununua kutokana na kutokuwa na elimu sahihi jambo linalohatarisha zaidi afya zao.


“Mtu mwenye ulemavu na mwenye kuhitaji kisaidizi cha kiti mwendo akipata kilicho sahihi kitamsaidia kukaa vizuri pamoja na kuendelea na shughuli zake za kila siku kwasababu haumii lakini akipata kisicho sahihi atapata madhara baada ya muda mfupi ikiwemo kupata ulemavu mwingine wa kupinda mgongo pamoja na vidonda mgandamizo hali inayoweza kumpelekea kifo,” Alisema Ndetembea.


“Mara nyingi tumeona viti wheel chair zisizo sahihi zinatolewa na watu wenye nia nzuri ya kuwasaidia walemavu lakini kwasababu hakuna elimu sahihi wanapewa visaidizi vinavyoenda kuweka maisha yao hatarini zaidi na kisichoendana na mazingira yao ambapo ndio sababu ya sisi kwa kushirikiana na taasisi ya TAI  Tanzania kuunda mradi huu wa JENGA JAMII JUMUISHI ili kuweza kukuza uelewa kati ya wadau  na watanzania wote,” Alieleza.


Aidha alifafanua kuwa jambo hilo litasaidia pale ambapo mtu atahitaji kiti mwendo  au mtu anatamani kusaidia kujua ni aina gani ya kisaidizi hicho anapaswa kununua kulingana na mahitaji ya muhusika pamoja na muongozo wa shirika la afya Duniani ili aweze kupata kiti mwendo sahihi na kinachoweza kurekebishika pale kinapoharipika.


Alisema kuna uhitaji mkubwa wa viti mwendo ambapo kama watu wataendelea kupata viti mwendo visivyo sahihi wengi wataendelea kubaki majumbani wakiwa wamefungiwa kwa  kushindwa kufanya shuguli za kiuchumi, kushindwa kwenda shule kwasababu tuu hawajapata kiti mwendo sahihi.


Kwa upande wake Abdullah Munishi kutoka shirika la maendeleo ya walemavu(TDDI) ambaye pia ni mtumiaji wa kitimwende alisema siku ya viti mwendo Duniani ilianzishwa mwaka 2008 na mtu ambaye alikuwa akitumia kiti mwendo ambapo aliona kuwe na siku maalum ya wao kusherehekea maisha wanayoyapitia ikiwemo changamoto walizozivuka na kuishi maisha ya kawaida.


“Tumetumia fursa hii kuelimisha lakini pia kuwa na muelekeo ni jinsi gani tunaweza kuishauri serikali kuhakikisha kwamba suala zima la upatikanaji wa viti mwendo sahihi na imara kulingana na mazingira ya kitanzania,” Alisema


Kwa upande wake mtaalamu wa viungo saidizi na viungo bandia kutoka hosipitali ya KCMC Sunday Haja alisema kuwa huduma hiyo bado iko nyuma haijapewa kipaumbele lakini uhitaji wake ni mkubwa kwani wahitaji sio wale wakuzaliwa na ulemavu tuu bali pia na wanaopata ulemavu kutokana na ajali hivyo jamii inatakiwa kujua kuwa huduma hiyo ni maalum kwani endapo mtu atapata kilicho sahihi italeta matokeo chanya kwenye maisha yake.


huo  alisema kuwa katika jamii kuna watu wengi wenye ulemavu na wanahitaji vifaa saidizi lakini upatikanaji umekuwa ni wa shida kwasababu mahitaji ni makubwa kulinganisha na upatikanaji wa vifaa hivyo ambapo sio sababu ya watu kutumia viti mwendo visivyo sahihi bali ni kutokana na kukosekana kwa elimu.


“Tumapaswa kuhakikisha kwamba familia za watoto au watu wenye ulemavu wanapata elimu na kutambua umuhimu wa wheelchair sahihi ni upi ili kuweza kuborsha maisha yao, kupandisha kujiamini pamoja na kuwasaidia kuzunguka kayika mazingira yao ambapo tunapendekeza sana viti mwendo vinavyotengenezwa hapa nchini kwasababu zinaweza kukabiliana na miunfombinu yetu lakini ni rahisi mtu kupimwa kulingana na alivyo na aina ya ulemavu alionao ndipo kikatengenezwa,” Alisema.


Mratibu wa huduma za utengemao kutoka wizara ya Afya Marine Shayo alieleza kuwa kumekuwa na changamoto ya watu kutumia viti mwendo visivyo sahihi na inatokana na kukosekana kwa muongozo wa usambazaji wa viti hivyo ambapo baadhi ya wanasiasa, vikundi na wasamaria wema wamekuwa wakitoa msaada wa visaidizi hivyo bila kuzingatia utaalamu hali inayopelekea watu kuwa na viti visivyokidhi mahitaji yao na kuwaletea madhara zaidi.


“Kama wizara, tunaendelea na kuandaa muongozo wa usimamizi wa vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu na utakapo kamilika utaondoa changamoto hii ya usambazaji holela wa viti mwendo na usiozingatia vigezo kwa asilimia kubwa,” Alieleza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI