Wananchi Wa kata ya Songosongo Wilayani Kilwa wameimizwa kujenga Tabia ya kufanya mazoezi kwa ajili ya kujilinda na magonjwa nyemelezi sambamba na kuimarisha Afya zao
wito huo umetolewa na Diwani wa kata ya songosongo Hassan Swalehe wakati wa mazoezi ya pamoja yaliyokutanisha vikundi mbalimbali vya Jogging huko wilayani kilwa ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa finali ya diwani cup unaotarajia kutimua vumbi hivi leo march 6/2024
amesema mazoezi yamekuwa chachu katika kuleta umoja, upendo na mshikamano hivyo wananchi wajitokeze katika kufanya mazoezi.
baadhi ya washiriki wa mazoezi hayo wamesema kwa kufanya mazoezi licha ya kuimarisha afya pia ukuza uchumi pamoja na kudumisha undugu.
0 Comments