Na Thobias Mwanakatwe, SINGIDA
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Mizengo Peter Pinda, anatarajia kuwa mgeni rasmi kesho Ijumaa (Machi 15, 2024) katika mkutano mkubwa utakaowashirikisha wafugaji wa nyuki zaidi 800 kutoka wilaya zoye za Mkoa wa Singia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kijiji cha Nyuki Co. Ltd, Philemon Josephat Kiemi, akizungumza na waandishi wa habari leo (Machi 14,2024) amesema kauli mbili ya mkutano huo ni kuwawezesha wafugaji wadogo wa nyuki wa Mkoa wa Singida kuuza asali na bidhaa zitokanazo na nyuki nje ya nchi ambazo zimekidhi viwango vya kimataifa.
Amesema mkutano huu ambao utakuwa ni wa pili kufanyika kwa kuwa Februari 2015 ulishawahi kufanyika mwingine ambapo wafugaji wa nyuki wapatao 500 ambao walishiriki mafunzo ya jinsi ufugaji nyuki kibiashara watagawiwa mizinga ya nyuki,vazi la nyuki pamoja na kifaa cha kuvuna vumbi la Singida ambayo ni miongoni mwa bidhaa mpya inayozalishwa kutokana na nyuki.
Kiemi amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo wafugaji wa nyuki wa Mkoa wa Singida watapitisha rasimu ya mwisho ya kuundwa kwa Umoja wa Wafugaji wa Nyuki Mkoa wa Singida ambao utakuwa na waanzilishi 800 kutoka katika kila kijiji na kata za mkoa hyu
Amesema kazi nyingine zitakazofanyika, mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Pinda atazindua kitabu kitakachojulikana Ifoneo Singida Philemon Kiemi na Kijiji cha Nyuki.Kitabu hicho kitaelezea historia ya maisha ya Philemon Kiemi na kijiji cha Nyuki kwani watu wengi wamekuwa wakiuliza maswali kwamba kijiji hicho kilianzaje na kinafanya nini ambapo majibu yote yatapatikana kupitia kitabu hicho.
"Tunaamini kuwa kama wafugaji wa asili wakipata vifaa vya kisasa kama vile mzinga wa Singida Techno Heifer na kuvuna mazao mapya kama vumbi la Singida pamoja na kupata vifaa vya kujikinga na nyuki wakati wa kulina asali sekta ya nyuki itapaa na kuwainua wananchi wengi nchini kiuchumi," amesema Kiemi.
Kiemi amesema jukumu kubwa ambalo kampuni ya Kijiji cha Nyuki italianate na inaendelea kulifanya ni kuwahakikishia wafugaji wa nyuki Mkoa wa Singida soko la uhakika soko la asali na bidhaa zinazozalishwa kutokana na nyuki katika kiwanda cha kuchakata asali ambacho kipo ndani ya Kijiji cha Nyuki.
Ameongeza kuwa lengo la kampuni ni kutaka kuwawezesha wafugaji wa nyuki waweze kuuza asali na bidhaa zitokanazo na asali kimataifa ambapo ili waweze kufikia hatua hiyo ni lazima wasajiriwe kufanya ufugaji wa nyuki hai (Organic Bee Keeping) ndipo wataweza kuuza asali na bidhaa katika masoko ya nje yakiwa na viwango vya kimataifa na kwa bei kubwa.
Kiemi amesema mkutano huo pia wamealikwa watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa vyana vya siasa,Wabunge wa mkoa wa Singida na wafugaji wa nyuki kutoka kampuni zilizopo katika mikoa ya Tabora,Manyara,Dodoma na. Arusha
0 Comments