Header Ads Widget

VIJANA MRADI WA YAM WAHOFU SOKO LA ZAO LA PARACHICHI KUPOROMOKA KUTOKANA NA ONGEZEKO LA WAKULIMA

 

Mkufunzi wa somo la Kilimo Cha Parachichi Aidan Kiwale akiwaonesha aina ya Parachichi washiriki wa mafunzo 

NA MATUKIO DAIMA APP 

VIJANA Mradi wa Youth Angecy Mufindi (YAM) wenye Ndoto ya kuwekeza kwenye  Kilimo Cha  zao la  Parachichi  wilayani  Mufindi  mkoa  Iringa  wamesema kutokana na mwamko  mkubwa  wa  wananchi  wengi   kuwekeza  katika  kilimo  cha  zao hilo  kuna  uwezekano  mkubwa  wa  soko la  Parachichi kuendelea  kuporomoka  zaidi iwapo serikali haitachukua  hatua  kutafuta   wawekezaji  wa  viwanda  vya  kuchakata   Parachichi ama  serikali  yenyewe  kujenga  kiwanda chake .



Kuwa  hadi  sasa   bei ya  Parachichi  kwa  kilo  moja  imeshuka  kutoka  kiasi cha  shilingi 18000 hadi  kufikia  kiasi cha  shilingi 1500 kwa  kilo hali  ambayo  ni  hatari  zaidi  kwa  mkulima  wa  zao  hilo la Parachichi  kupata  faida  kwa  kilimo  hicho .



Akizungumza  wakati  wa  mafunzo ya Kilimo kwa  vijana   wa  mradi wa Youth Angency  Mufindi (YAM) Leo   katika  ukumbi  wa  Yatima  Igoda kata  ya  Luhunga mkufunzi  wa mafunzo hayo Aidan  Kiwale  alisema awali  wakulima  wa zao la Parachichi walikuwa  wakitegemea zaidi kilimo  hicho  kuliko  mazao  mengine ya  biashara  kutokana na kuwa na soko la uhakika na wanunuzi  walikuwa  wakifika  hadi  shambani ila sasa  imekuwa  tofauti hasa  upande wa  bei .


Kwani  alisema  msimu wa mavuno ya Parachichi  ndio  kwanza  umeanza  hivyo walitegemea  mwanzo wa mavuno  bei  kuwa  nzuri  zaidi ila matokeo yake  wameanza na mwanzo mbaya  kwani  kilo ni Tsh 1500 tofauti na mwaka jana   walipouza  kilo moja hadi  kiasi cha shilingi 1800 na maeneo mengine waliuza  hadi  shilingi 2000.


Hivyo  alisema  imani  kubwa kwa  wakulima wa zao hilo  ipo mikononi mwa  serikali  kupitia  wizara ya  viwanda kuona  inawatafuta  wawekezaji  zaidi watakaofanya  uwekezaji katika  sekta ya mazao ya matunda hayo ya Parachichi  ili  kumwezesha mkulima kupata  faida  kama  ilivyo maeneo mengine  ambayo  yafanya  vizuri katika  uzalishaji wa mazao ya  biashara .


Kiwale  alisema  pamoja na kilimo  cha Parachichi  kwa  wilaya  ya Mufindi kuendelea  kushika kasi kwa  kila mwananchi  kutamani  kuwekeza katika kilimo  hicho ila wasiwasi  wao ni kuendelea  kupata  soko la uhakika  la  zao hilo .


" Imani  yetu  kubwa  kwa  mheshimiwa  Rais Dkt  Samia  Suluhu Hassan  kama  alivyofanya  jitihada kubwa ya  kutujengea  barabara  ya  lami  kutoka  Sawala  hadi Iyegea na  kutufanya  wakulima  kusafirisha mazao  yetu  kwa  urahisi  zaidi  tunategemea   kilio  chetu  cha kiwanda  cha kuchakata  zao la Parachichi  kikajengwa katika mkoa  wetu ili kumkomboa mkulima "  alisema Kiwale 


Kuwa  nguvu kubwa imefanywa na mradi wa YAM  kuwapatia  elimu   vijana  toka  familia  zenye mazingira  magumu na  mwitikio  wa  vijana  hao  kuwekeza katika  kilimo cha Parachichi ni mkubwa  zaidi hasa  kutokana na faida  kubwa  iliyopo katika  kilimo  hicho  ukilinganisha na kilimo cha mazao ya mengine kama  mahindi na nyanya .


Kwani  alisema  mti  mmoja wa  Parachichi iwapo utatunzwa  vizuri unaweza na  kulimwa  kwa  kitaalamu  kwa  kipimo  cha mita 10 kwa  10 katika eka mmoja utakuwa  na  mita 40  baada ya  miaka  mitatu  kwa  baadhi ya  mbegu  utakuwa na wastani  wa matunda 1000 kwa miti  10  pekee   hivyo kwa  miti 40 utakuwa na jumla  ya matunda 40,000 na  mti  huo  huo mmoja  ukifika baada ya  miaka  minne ama mitano unaweza  kutoa matunda 1200 na  hivyo kuwa na uhakika  wa kupata  milioni 1  kwa miti  10  kwa  mwaka mzima tofauti na mkulima  wa zao la Mahindi  .



"  Leo  wewe  mkulima wa Parachichi ukiuza  unaweza kwenda  kununua mahindi utapata madebe  150 kwa kuuza  matunda yako  miti  10  pekee hivyo  zao  hilo  linalipa japo  linaweza  kulipa  zaidi kama bei  elekezi  ya  serikali ikatolewa "


Tofauti na mazao  mengine  zao  hilo la Parachichi ni  zao  lenye  faida  kuwa  iwapo  kama  kutakuwa na soko la uhakika   na  kuwa na bei  elekezi  ya serikali katika  zao hilo  isiwe  mfanyabiashara  analipa kwa kujisikia  yeye na sio matakwa ya  mkulima .


Washiriki  wa mafunzo hayo  Ester  Kahama  kutoka kata  ya Ihanu  alisema  elimu  aliyopata  ya  kilimo cha Parachichi  itapelekea  kuongeza  ufanisi  zaidi  tofauti na kilimo cha mazoea ambacho  alikuwa akilima  awali .

Japo alisema Kasi ya Wakulima itashusha bei ya zao hilo hivyo ni vema mazingira ya uhamasishaji Kilimo Cha Parachichi yaende na uhamasishaji wa uanzishwaji viwanda vya kuongeza thamani ya zao hilo.


Alisema kupitia mradi  huo wa YAM ameweza  kupata  elimu ya  kutosha ya  kilimo  bora  cha Parachichi na kuwa hivyo  si  tu atakwenda  kuongeza  kasi ya  uzalishaji  bali  atakuwa  mwalimu mzuri  kwa  wananchi  wa kijiji na kata  anayotoka .


Huku  kijana  Nehemia  Mkusi  kutoka  kijiji cha Ispii Ihanu  alisema   wamejifunza  faida ya  kilimo cha Parachichi  pamoja namna  ambavyo  kilimo  hicho  kinavyoweza kumkomboa  kijana .


Mafunzo hayo  ya  kilimo  na ujasiriamali kwa  vijana  yameendelea  kutolewa na Halmashauri ya wilaya ya  Mufindi Mufindi chini ya mradi wa Foxes  Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland mradi  unaotekelezwa kwenye kata za Mdabulo ,Luhunga na Ihanu katika  wilaya ya Mufindi huku lengo la  mradi  lilikuwa kuwafikia  vijana   320 ila  hadi  sasa  toka  mradi ulipoanza  mwaka 2021 tayari wanufaika 420 kwa vijiji  vyote  16 wamefikiwa .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI