Header Ads Widget

RAIS WA WACHIMBA MADINI FEMATA JOHN BINA AFUTURISHA WACHIMBAJI NA JAMII YA WAISLAMU MKOANI SINGIDA

 


Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji Madini Tanzania FEMATA John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati Tendaji ya FEMATA ameungana na jumuhia ya Waislamu Wachimbaji wa Mkoa wa Singida katika Dua maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake nchini aongoze kwa amani na utulivu.


Dua hiyo maalumu imefanyika Nyumbani kwake Mkoa wa  Singida larehe 30 Machi 2024. ambapo Rais huyo alijumuika na baadhi ya wana chama wa REMAs ya SIREMA, Viongozi wa dini wakimemo  Masheikh katika kupata Futari  aliyowaandalia na Rais huyo FEMATA.


Futari hiyo ambayo pia ilijumuisha watu wenye mahitaji maalumu Yatima, Wajane na wazee wa eneo hilo la mjini Singida.


Rais wa FEMATA amelenga kujumuika na Viongozi wa Dini pamoja na wachimbaji hao kama hatua ya kuonesha mshikamano na umoja katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


"Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya yaliyomema mbele za Mungu wetu tuombee Shirikisho letu la FEMATA kwa kuwaombea Wachimba madini na bila kumsahau kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu" amesema Rais Bina. 


Kwa kuwa Rais wa FEMATA ni Mkazi wa Singida yupo karibu na wachimbaji, Wananchi na Viongozi wa Dini ameamua kuandaa futari hiyo ili kujumuika na wachimbaji, Wananchi na majirani zake kufanikisha ibada hiyo muhimu.


Awali ya kwenda kushiriki futari hiyo Rais wa FEMATA amepiga ROLLER kama  mchimbaji katika Mgodi wa wachimbaji wadogo wa Matogo na kiongozi huyo kwa upendo mkubwa kama mchimbaji ameonesha uwezo wa kupiga Roller.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI