Header Ads Widget

SHIRIKA LA SAUTI YA HAKI TANZANIA LIMETAOA MITAJI YA BIASHARA KWA WANAWAKE KUMI MKOANI IRINGA

 

 

 

Shirika la Sauti ya Haki Tanzania limetoa mitaji ya fedha kwa wanawake 10 wakazi wa mtaa wa Mibata kata ya Nduli, manispaa ya Iringa, ambao wanajishughulisha na kazi ya kupika na kuza pombe za kienyeji ili kulea familia zao, lengo likiwa ni kuwezesha wanawake hao kufanyabiashara nyingine za kiuchumi na kupata muda kulea familia zao ili kupunguza udumavu na ukatili kwa Watoto .

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha hizo, Mkurugenzi wa sauti ya haki Tanzania, Wakili Leticia Petro Ntagazwa, amesema matumizi ya pombe za kienyeji ndani ya mkoa wa Iringa yamezidi kushika kasi jambo ambalo linaathiri makuzi na usalama kwa Watoto, jambo ambalo linachangia Watoto wengi kukataa shule na kujiingiza katika matumizi ya pombe wakiwa na umri mdogo.

 

Amesema, anaamini Mitaji hiyo itakwenda kubadilisha Maisha ya wanawake hao kwa kuanzisha biashara mbadala na uuzaji wa Pombe za Kienyeji, jambo ambalo litawezesha kuwa na muda wa kulea familia zao vyema.

 

Aidha Waikili Letiaci Petro Ntagazwa, amewakumbusha wanaume kusimamia majukumu yao ya kulea familia ili kupunguza wimbi la Watoto wanaopitia changamoto za ukatili kutokana na wanawake kuachiwa majukumu yote hivyo kukosa muda wa kuangalia Watoto wao.

 



Katika hatua nyingine amewakumbusha wazazi na walezi kuwa natabia ya kuzungumza na Watoto wao mara kwa mara ili kuweza kutambua changamoto wanazozipitia hasa pindi wanapokuwa mbali nao, kwani itasaidia kupunguza ukatili kwa Watoto.

 

Naye Afisa kutoka  mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kanda ya Nyanda za juu kusini, Adrick Simon Ndelwa, amesema kwa sasa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuja na mbinu mpya za kusafirisha dawa hizo kwa kutumia vyakula kama biscuit, cake na vyakula vingine jambo ambalo linafanya kufikiwa na kutumiwa na Watoto wadogo, hivyo kuwataka wazazi na walezi kuwa makini na Watoto wao kwa kuwaonya juu ya kupokea vitu kutoka kwa watu wasio wafahamu.

 

Kwa upande wao wananchi walioshiriki sherehe hizo wamelishukuru shirika hilo kwa kuendelea kuwasaidia wakazi waneo hilo katika Nyanja mbalimbali hasa ushauri wa kisheri Pamoja na elimu za ujasiriamali.

 

Prisca Lameck, mkazi wa mtaa wa Mibata kata ya Nduli, amesema tatizo kubwa linalo wakabili Watoto wa eneo hilo ni wazazi wao kushinda vilabuni kutokana na kufanyabiashara ya pombe za kienyeji au kuwa wanywaji wa pombe hizo hivyo kupelekea Watoto wengi kuingia kwenye makundi hatari kutokana na kukosa maelezi ya wazazi.

 

Naye Diwani wa kata ya Nduli Bashiru Mtove, amelishukuru shirika la sauti ya haki Tanzania kwa kuendelea kuisaidia jamii kwa kutoa elimu Pamoja na mitaji ya biashara kwani jambo hilo limekuwa na msaada mkubwa sana kwa watanzani.

Shirika la sauti ya haki Tanzania limeanzishwa mwaka 2016 lengo likiwa ni kulinda, kutetea na kuhamasisha haki za wanawake na Watoto na kwa sasa linafanya kazi mbalimbali kama elimu ya haki za wanawake na Watoto, msaada wa kisheria, elimu ya ukatili wa kijinsia, elimu ya mazingira na kutunza mazingira, elimu ya kijinsia na ya mabadiliko ya tabia nchi Pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia miradi mbalimbali kama vile ufugaji wanyuki, na mikopo midogo midogo kwa wanachama.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI