Header Ads Widget

SHAMBA LA MKULIMA LAGEUZWA ATM CARD

 .






JINSI SHAMBA LA MKULIMA LILIVYOGEUKA ATM KWENYE TAASISI ZA KIFEDHA.

-MAZAO RAFIKI,KAHAWA,NDIZI,PARACHICHI NA MAKADEMIA YAZIDI KUSTAWI.

JAMII nchini hasa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali wametakiwa kujiingiza kwenye kilimo cha mazao mbalimbali yaliyo kwenye soko la uhakika ili kujiingizia kipato na kuondokana kute gemea ajira itakayowachelewesha,,,anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 14/2024 na mkulima maarufu wa mazao mbalimbali wa kijiji na kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe,Tinson Nzunda wakati akizungumza na waandishi wa habari shambani kwake.

Nzunda amekuwa kivutio kwa wakulima wengine baada ya mashamba yake yenye hekari zaidi ya 60 kushamiri huku akitarajia kuvuna kwa miezi tofauti na kujiingiza kipato kikubwa  baada ya kulima kitaalam mazao ya Parachichi,Ndizi,Kahawa na Makademia.

Nzunda ambaye ni diwani wa kata ya Nyimbili na mkulima maarufu mkoani humo,amesema amelima mazao ya Makademia (Karanga pori) parachichi,ndizi na kahawa ambapo migomba imetoa ndizi na ameamza kuvuna na kuuza akijiingiza kipato.

Amesema baada ya kuvuna ndizi anaendelea kuziuza ambapo kwa wiki mbili ameingiza Tsh,Milion 1.4 huku akitarajia kuvuna kahawa mwezi ujao na baada ya miezi mitatu mbele atavuna makademia huku shamba lake likibatizwa jina kuwa ATM Card.

Ameongeza kuwa kutokana na kilimo cha mazao hayo kuwa na soko la uhakika amewataka wananchi hasa vijana wanaomaliza vyuoni wajiingize kwenye kilimo cha mazao hayo wakati wakisubiri ajira ili waendelee kuendesha maisha yao na familia zao.

‘’Imekuwa ni kawaida vijana wengi wanaohitimu vyuo,wakikaa vijiweni wakisubiri kuajiriwa badala ya kujiingiza kwenye ujasiliamali ikiwemo kilimo hali inayopelekea waishi maisha magumu,amesema Nzunda.

Aliongeza kuwa maparachichi yanakamuliwa mafuta soko lake lipo Ulaya,Kahawa soko lake lipo kwenye mnada wa pamoja,Tanzania Cofee Bord,(TCB) Makademia au karanga pori soko lipo maeneo mbalimbali nchini hivyo ni bora vijana wakaingia kwenye kilimo cha mazao hayo.

Mwamvita Samwel mkazi wa ,Mbozi,amesema nayafahamu mashamba ya Nzunda na kusema ni ATM Card kwani kila anapoingia kuchuma zao furani anavuna fedha,na kuwa kuna kila sababu ya kujifunza kwake ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI