Na Fredy Mgunda, Iringa.
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimesema kitampisha kiungozi anayekubarika kwa wananchi ambaye hana makandokando yoyote kwa lengo kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote.
Akizungumza wakati ziara ya Secretarieti ya Mkoa,Katibu siasa uenezi na mafunzo Mkoa wa Iringa neno Itikadi halipo Joseph Ryata aliwaambia viongozi wa ngazi za chini wa chama hicho kuwa wao ndio wanaishi na wanajua viongozi bora hivyo sio sahihi kupendekeza au kumpigia kampeni mgombea ambaye hafai.
Ryata alisema kuwa CCM inahitaji ushindi kwa namna yoyote ile lakini lazima wawe na viongozi waliobora na wanaokubarika na wananchi ambao ndio wapiga kura za mwisho kujua nani kiongozi wa mkoa wa Iringa.
"Iringa hatutaki kusikia kitongoji,mtaa, kijiji au kata imeenda upinzani wanaccm lazima tuwe makini na kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan ambaye ndio mwenyekiti wetu wa CCM kwa kumchagulia viongozi walio bora ambao wataliongoza taifa la maendeleo kwa kila mtanzania" alisema Ryata
Alisema kuwa viongozi wa CCM ukimuangalia tu unajua huyu kiongozi hivyo wanaccm wa mkoa wa Iringa lazima wawe makini kuchagua viongozi makini ambao wanachagulika kwa vyama vyote.
Nao baadhi ya Makada wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa walisema kuwa wanaunga hoja na katibu wa siasa na uenezi, itikadi na mafunzo mkoa wa Iringa namna ya kuwapata viongozi ambao wanachagulika na wananchi wa vyama vyote.
0 Comments