Header Ads Widget

RAIS DK. MWINYI AKEMEA VIONGOZI NA WATENDAJI WANAOTUMIA OFISI ZA UMMA KWA MASLAH YAO BINAFSI

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi na  watendaji wa taasisi za umma kuacha mara moja kutumia ofisi na dhamana zao kwa maslahi yao  binafsi na endapo wakibainika hatua kali za kisheria watachukukiwa dhidi yao.

Rais Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo leo katika hafla ya kuadhimisha miaka mitatu ya kuanzishwa kwa mfumo wa Sema na Rais (SNR) iliyofanyika katika Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja Mjini Magharibi Unguja Tarehe; 16 Machi 2024.

Amesema, ni vyema viongozi na watendaji wa Serikali waache kuzitumia ofisi na dhamana zao kwa maslah yao binafsi kwani ni kukosa maadili ya utumishi wa umma na ikithibitika watachukuliwa hatua kwa mujibu  kisheria bila ya kumuonea mtu.

"Kwa kuzingatia kuwa binafsi nayaona masuala yote yanayowasilishwa kupitia mfumo wa SNR, natumia fursa hii kuwatanabaisha viongozi na watendaji juu ya taarifa zinazotumwa dhidi yao kuhusiana na masuala yaliyo kinyume na maadili ya uongozi yakiwemo yanayohusu mahusiano na kukosa uadilifu," ameeleza Rais Dk. Mwinyi.

Rais Dk.Mwinyi amewakumbusha watendaji hao kuvitunza  vitendea kazi walivyokabidhiwa na Serikali na kutumia  katika kuwafikia wananchi  kwa urahisi, kuwasiliza, kuwahudumia na kufuatilia na kutatua changamoto zinazowakabili.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa, bado kuna kazi ya kufanya kuhakikisha mfumo wa Sema na Rais unaleta mafanikio yanayotarajiwa

"Kitengo cha SNR kina wajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa kutumia njia mbalimbali kwa Wananchi ili waweze kutumia vyema mfumo huu kwa madhumuni yaliyokusudiwa," ameeeleza.

Pia ametoa wito kwa Watendaji wa Sema na Rais kuzidisha ushirikiano na Wizara na Taasisi zote hasa zile zenye idadi kubwa ya malalamiko ambayo yanakaa kwenye mfumo bila ya kupatiwa ufumbuzi.

Katika hatua nyingine Rais Dk. Mwinyi amewaomba Wananchi waendelee kutumia vyema mfumo wa Sema na Rais kueleza changamoto za na kutoa ushirikiano kwa watendaji ikiwemo kutoa taarifa kwa usahihi na ufafanuzi pale zinapohitajika.

Mapema Naibu Mkurugenzi wa Sema na Rais (SNR), Haji Khamis Makame amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo huo umesaidia kuongeza Uwajibikaji na ufanisi kwa Watendaji wa taaisis za Serikali pamoja na kuondosha Urasimu katika upatikanaji na utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Ameeleza kuwa, kwa mwaka 2020/2021 mfumo umepokea malalamiko 6,773 na wametatua malalamiko 4,571 na malalamiki 2,202 yanaendelea kufanyiwa kazi sawa na asilimia 67.5 huku Mwaka 2022/2023  malalamiko yalipokelewa ni 10,081 na Malalamiko 7,871 yamepatiwa ufumbuzi huku malalamiko 2190 yanaendelea kupatiwa ufumbuzi sawa na asilimia 78.3.

"Kwa mwaka 2023/2024 mfumo tumepokea jumla ya malalamiko 13517 na malalamiko 11116 yamepatiwa ufumbuzi huku kesi 2351 yanaendelea kufanyiwa kazi kwa hatua mbalimbali sawa na asilimia 82.6," ameeleza Naibu Mkurugenzi Sema na Rais.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Ali Suleiman Ameir amesema, miaka mitatu ya mfumo wa Sema na Rais umewafikia wananchi katika shehia zote za Unguja na Pemba.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI