Header Ads Widget

KAMATI YA BUNGE PIC YATEMBELEA MIRADI YA GESI ASILIA MTWARA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) imefanya ziara mkoani Mtwara na kutembelea miradi ya gesi iliyopo Msimbati na Madimba. 


Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Ombeni Sefue amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa taifa ambapo asilimia 65 ya gesi hutumika kuzalishia umeme nchini. 


Amesema kuwa gesi hiyo inatumika kuzalishia umeme nchini ambapo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi.

 

“Tumefarijika kupata fursa ya kuwaonyesha wawakilishi wa wananchi fedha za taifa hili zinavyotumika na mchango inayotolewa katika uchumi wa nchi kama mlivyosikia asilimia 65 ya umeme unaotumika nchini unatokana na gesi asili ya Songosongo na Mnazibay  tumekabidhiwa jukumu hili kubwa kwa Taifa” amesema Sefue


Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Clement Sangu Mbunge wa Jimbo la Kwela Zanzibar amesema kuwa ziara hiyo ni ziara maalum ya kibunge ambayo imeanzia mkoani Tanga katika mradi wa bomba la mafuta. 


“Serikali inafanya kazi kubwa na mabadiliko tumeyaona kwa kiasi kikubwa tunapongeza uwekezaji huo ambapo awali 2019 kulikuwa na wawezekezaji watatu akiwemo TPDC ambapo kwa sasa tumeingia katika rekodi ya nchi ambapo tunamiliki hisa kwa asilimia 40 kwenye miradi ya gesi ambapo 60 zinabakia kuwa za mwekezaji” amesema Sangu

“Kwenye huu ubia serikali imeweka zaidi ya shilingi bilioni 104.6 ambapo sasa TPDC anaingia kwenye uzalishaji wenye tija sasa ambapo asilimia 65 inaenda kuzalisha umeme hasa ukizingatia kuwa sasa matumizi yamekuwa makubwa nchini” amesema  Sangu


Nae Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya PIC Vuma Agustino  amesema kuwa uwepo wa Tanzania kwenye miradi ya  uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia nchini unaonyesha kuwa tumepiga hatua kubwa.

“Tunasifu uwepo watanzania hasa vijana kwenye maeneo ambayo tumetembelea yote tumeona watanzania ambapo awali serikali ilikuwa ikitumia fedha nyingi kuwalipa ambayo baada ya serikali kusomesha watanzania na pia nafasi zote zimeweza kuchukuliwa” amesema Augustino

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS