Header Ads Widget

BREAKING: AJALI YAUA WAANDISHI WA HABARI WAWILI WA MKOA WA LINDI

 

Hii ni Moja kati ya ajali mbaya iliyosababishwa na uzembe wa Madereva Haina uhusiano na ajali hii picha na mtandao

NA MATUKIO DAIMA APP 

WATU wawili ambao ni waandishi wa habari mkoa wa Lindi  wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali .


Ajali hiyo iliyohusisha gari dogo imetokea majira ya usiku wa  kuamkia Leo March  26 eneo la  Nyamwage mkoani mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)


Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea  Dar es Saalam  kwenye mafunzo kurejea mkoani   Lindi .

Waandishi waliofariki dunia ni Abdalla Nanda wa Chanel Ten mkoa wa Lindi na Josephine Kibiriti wa   Sahara Media Group.M


Matukio Daima media amemtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)Protasi Mutayoka  ambae amethibitisha kutokea Kwa Ajali na kuwa Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 7 usiku wa March 26 na Chanzo ni Dereva wa Centar ambae baada ya ajali alikimbia na msako wa kumtafuta unaendelea.

Alisema kuwa kwenye gari ndogo ya waandishi walikuwa watu watatu na Wawili Mwanamke mmoja na mwanaume walifariki Dunia eneo la tukio na mmoja ni majeruhi amelazwa Hospitali na mguu wake mmoja amevunjika .

VIDEO :FULL HII HAPA

Kamanda huyo alisema eneo la ajali ni eneo nzuri Haina changamoto ya miundo Mbinu huku akitoa onyo Kwa madereva kufuata Sheria za usalama barabarani.

MATUKIO DAIMA MEDIA TUNATOA POLE NYINGI KWA FAMILIA PIA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA LINDI NA WAANDISHI WOTE  NCHINI KWA MSIBA HUU TULIWAPENDA SANA WANA TASNIA WENZETU ILA MUNGU KAWAPENDA ZAIDI YETU HIVYO TUSEME NINI BASI BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE NA LIHIMIDIWE .


AMEN



Post a Comment

1 Comments

  1. Hakika sisi ni wake Mwenyezi Mungu na Hakika kwake tutarejea, Abdalla amefariki na Funga yake, Allah aijalie funga zake ziwe mwanga na muombozi kwenye maisha yake ya milele👏

    ReplyDelete



MAGAZETI



BBC NEWS