Header Ads Widget

MFANYABIASHARA GHULAM NA WENZAKE 11 WAFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

 

 


Jumla ya watuhumiwa 12 akiwemo mfanyabiashara Ghulam Rasoul  Abrahimu Mia wamefikishwa Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa kwa tuhuma 6 ikiwemo ya uhujumu Uchumi na utakatishaji  fedha kwa kujipatia lita za mafuta aina ya Disel lita laki saba na Hamsini na tatu zenye thamani ya kiasi cha shilingi bilioni mbili nukta mbili.

 

Watuhumiwa  hao  12  walifikishwa  jana  mbele ya  hakimu mfawidhi  wa  mahakama  ya  mkoa  wa  Iringa  Hororius  kando   wakisomewa  makosa  6  huku  kosa  moja   la   utakatishaji pesa  kwa  kujipatia mafuta  aina  ya disel  lita  705,300 zenye  thamani  ya  Tsh  bilioni 2,292,075,944.60 ambapo  watuhumiwa hao  wakabiliwa na  kesi ya  uhujumu  Uchumi   namba 5001 ya  mwaka  2024.

 

Kosa  la  kwanza  walilosomewa  wote ni kuongoza  gege la uhalifu  kinyume  na  kifungu  namba 57 na  kifungu  namba 60  cha  sheria ya  uhujumu Uchumi wakati  kosa la  pili  uharibifu  wa mali  kinyume na kifungu  namba  326 cha  sheria  ya  makosa  ya  jinai  .

 

 Huku  kosa namba  3 ni  wizi   kinyume na kifungu  namba  258 na 255 cha sheria  ya  makosa  ya jinai  na  kosa la nne ni  kuisababishia  hasara  mamlaka  kinyume na na  kifungu  cha 57 na 60  ya  sheria  ya  uhujumu  Uchumi   huku  kosa  la  sita  ni utakatishaji  wa pesa .

 

Upande  wa  washtakiwa  wanatetewa na mawakili  watatu  akiwemo Barnabas Nyalusi, Moses  Ambwindwile  na Stanley Nyamley  huku  upande  wa jamhuri kukiwa na mawakili  watatu .

 

Kesi   hiyo  itatajwa tena  March 25  mwaka  huu  na  watuhumiwa  hawakutakiwa  kujibu  chochote  na  kurudishwa  mahabusu, kwa  kuwa mahakama  hiyo haina   nguvu kisheria .

 

……………

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI