Header Ads Widget

TAASISI YA IGT NA BASIS YA UGANDA ZAZINDUA MRADI WA JET MINERALS GRAND CHALLENGE

 




TAASISI  ya Initiative for Good Governance and Transparency in Tanzania (IGT) kwa kushirikiana na Shirika la BASIS International ya Uganda wazindua mradi wa JET Minerals Grand Challenge unaolenga kuzuia rushwa kwenye sekta ya madini.


 Mkurugenzi wa Shirika la IGT Edwin Soko amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwenye Nchi nne za Maziwa Makuu, ikiwemo Uganda, Tanzania, Zambia na DRC.

 Soko alisema kuwa IGT kwa hatua za awali za.kuutambumisha mradi huo wamefanya ziara kwenye ofisi za wadau mbalimbali ikiwemo msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali, tume ya haki za binadamu,  TAKUKURU,  Taasisi za kihabari, Taasisi zinazojishughukisha na madini  kwa lengo la kuwajengea uelewa wa mradi huo ili baadaye washirikiane kwa pamoja.


"Mradi huu unalengo  la kutengenezeza jukwaa la.mtandaoni la kupokea taarifa za siri za rushwa pasipo kumtaja mhusika  ili kupunguza rushwa kwenye sekta ya madini."


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI