NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Zoezi hilo lililozinduliwa wiki iliyopita linatarajiwa kuzifikia kata zote za mkoa wa Kilimanjaro ambapo mpaka sasa wameshazifikia kata tatu.
Akizungumza Jackline Malya mkazi wa kitongoji cha Kiareni kata ya Okaoni alisema kuwa, kitongoji chao hakijafikiwa na huduma ya umeme lakini ujio wa Mobile clinic sasa wanamatumaini ya kufikiwa na huduma hiyo.
Jackline alisema kuwa, kitendo cha Watumishi wa Tanesco wakiongozwa na Meneja wa mkoa kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kusikiliza kero ni jambo ambalo linapaswa kuingwa na mashirika mengine ya umma.
"Wananchi tunayo matatizo mbalimbali lakini tunashindwa kutambua tuyapeleke wapi hivyo kuja kwa watumishi hawa katika maeneo yetu inatupa fursa kueleza matatizo yetu na kuyapatia ufumbuzi hivyo taasisi nyingine zinapaswa kuiga hili jambo" Alisema Jackline.
Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha Kiareni, Rafael Malya alisema kuwa, toka nchi ipate Uhuru kitongoji hicho hakijafikiwa na huduma ya umeme lakini kupitia huduma ya Mobile clinic sasa wanatarajia kufikiwa na huduma ya umeme.
Malya alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi ambazo amekuwa akizifanya ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
"Kitongoji chetu hakijawahi kufikiwa na huduma ya umeme lakini leo kupitia huduma hii wa Mobile clinic watumishi wa Tanesco wamefika katika kitongoji chetu na kufanya savei hivyo ni matumaini yetu huduma hii tunaenda kuipata mapema" Alisema Malya.
Mwisho..
0 Comments