Home
About
Contact
Header Ads Widget
Home
News
Entertainment
Sports
Magazeti
Home
kitaifa
JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WA KAKA YAKE WA MIAKA KUMI.
JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WA KAKA YAKE WA MIAKA KUMI.
Misalaba
Wednesday, March 13, 2024
Na Fredrick Siwale - Matukio Daima APP Mufindi Iringa. Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 Jela mshitakiwa Rodrick Msilwa (20) kwa kosa la kubaka mtoto wa kaka yake ambaye jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 10. Awali akimkumbushia mashitaka yake mtuhumiwa ,Mwendesha mashitaka wa Serikali Mh.Twide Mangula aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo desemba 12 mwaka 2023 na kusomewa shitaka lake ambalo alikana . Mh.Mangula aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili kukomesha tabia iliyozuka ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto kwa kuwalawiti na kuwa baka . Aliomba Mahakama kutoa adhabu kulingana na tendo la ubakaji kwa mtoto huyo lilivyofanyika mchana kweupe kitendo ambacho kitaweza kumathiri vibaya mhanga huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kulingana utoto wake. Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mufindi Mh.Benedick Nkomola alisema Mahakama bila shaka yoyote imeona mshitakiwa ametenda kosa kulingana na ushahidi uliotolewa na Mhanga ni wazi kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo la ubakaji dhidi ya Mhanga . Aliongeza kuwa Mahakama imepokea na kutathimini Mhanga anapotoa ushahidi na imejiridhisha kwamba Mhanga alichoongea ni kweli rejea kifungu 127 (7) sheria ya ushahidi sura ya 16 REKEBU ya 2022. Akihitimisha kusoma hukumu Mh.Nkomola alisema Mahakama imeona kuwa Mshitakiwa ametenda kosa la ubakaji dhidi ya Mhanga na kumtia hatiani Mshitakiwa kwa kosa la kubaka lililopo kifungu 158 (1) sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 REKEBU la 2022 , Mahakama imemtia hatiani Mshitakiwa kwa kuzingatia pia kifungu 235 (2) sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai ,sura ya 20 REKEBU la 2022. ..........mwisho..............
Post a Comment
0 Comments
MAGAZETI
NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI
TV News
World News
UZA NUNUA NASI LEO
Subscribe Us
MATANGAZO
TIBA YA UKANDAJI WA MGONGO, KICHWA KUTOKA NEEMA BEAUTY, SPA SALOON
MAKALA NZURI ZAIDI
MEZA, YA MAGZETI LEO JUMATANO JULAI 9/2025:DIRA YA TAIFA 2050 YAKAMILIKA , RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI JULIA 17,RC SIRRO AWAONYA WATUMISHI KIGOMA
MATUKIO DAIMA TV ONLINE
Wednesday, July 09, 2025
STAY CONNECTED WITH US
Ad Space
Responsive Advertisement
Most Popular
WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MITWERO WAIPIGA JEKI SHULE MADAWATI
Friday, July 04, 2025
WANAWAKE MORO WAAMKA KWA KISHINDO KUCHUKUA FOMU ZA UDIWANI
Friday, July 04, 2025
MKE WA BALTASAR WA VIDEO 400 ZA NGONO ,VIDEO YAKE YANASWA NA MUME MWINGINE
Saturday, November 09, 2024
Contact form
0 Comments