Header Ads Widget

CCM YASHINDA UDIWANI KIGOMA UJIJI

 


Msimamizi wa uchaguzi katika manispaa ya Kigoma Ujiji Mwantumu Mgonja (kulia)

Akikabidhi cheti kwa mgombea wa CCM Mlekwa Kigeni ambaye  amekuwa mshindi wa  matokeo ya udiwani kata ya Kasingirima

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kiti cha udiwani katika kata ya Kasingirima Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya mgombea wa chama hicho Mlekwa Mfamao Kigeni kufanikiwa kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo w nafasi ya udiwani kwenye kata hiyo.

 

Msimamizi wa uchaguzi huo, Mwantumu Mgonja kwa niaba ya Tume ya Taifa ya uchaguzi alimtangaza Mlekwa Kigeni  wa CCM aliyeibuka aliyeibuka mshindi baada ya kupata kura 437.

 

Mgonja alimtangaza  Ahamad Alumbula  wa ACT Wazalendo aliyepata kura 233 katika uchaguzi huo ambao vyama 12 vilisimamisha wagombea huku kukiwa hakuna mgombea mwingine yeyote aliyekuwa na kura Zaidi ya 10

 

Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa Jumla ya wapiga kura 713 walijitokeza katika uchaguzi huo kati ya wapiga kura 1960 walioandikishwa ambapo kura halali zilikuwa 699 na kura 14 zikikataliwa.

 

Wakati muda wa mwisho wa kufunga vituo ukikaribia ikiashiria kumaliza kwa upigaji kura iliibuka vurugu katika kituo cha mtaa wa Livingstone ambapo viongozi wa chama cha ACT na wanachama wao walitangaza kukamata kura zilizokuwa na nia ya kuingizwa kunyemela hali iliyosababisha vurugu na viongozi wa ACT kukamatwa.

 

Katibu Mwenezi wa ACT mkoa Kigoma,Azizi Mussa alithibitisha kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa,Abdul Nondo na mgombea udiwani,Ahamd Alumbula ambao hadi usiku walikuwa wanashikiliwa kituo kikuu cha polisi mjini Kigoma.

 

Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Abdallah Kiembe aliyepata ajira ya serikali katika halmashauri ya Kondoa mkoani Dodoma.


Mlekwa Mfamao Kigeni wa CCM mshindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kasingirima Kigoma Ujiji mkoani Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI