Header Ads Widget

MAJALIWA -WATUMISHI WMA FANYENI UKAGUZI WA VIPIMO MARA KWA MARA

  

NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA APP DODOMA 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa,amewaagiza watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) kusimamia vyema sheria pamoja kanuni zake na kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa vipimo mara kwa mara katika maeneo mbalimbali.


Majaliwa, ametoa maagizo hayo leo jijini hapa, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa jengo la makao mkuu ya wakala huo nchini.


Amesema kama watumishi hao watakuwa wanafanya kaguzi za mara kwa mara itamsaidia na kumlinda mlaji na mnunuaji kwani wafanyabiashara wamekuwa wakiwaibia wananchi kupitia mizani hasa kwenye maduka


"Niwatake wafanyabishara nchini kuzingatia vipimo na kuacha tabia ya kujinufaisha kwa kuwaibia wengine, " Amesema .


Na kuongeza kusema "Wafanyabiashara acheni kulegeza vipimo vilivyowekwa, acheni kuwaibia wengine na wanachi tunabidi kuwa wajanja kila tumapohitaji bidhaa lazima kuzingatia ujazo kwa mujibu wa vipimo vilivyowekwa kisheria"amesema.


Pia Waziri ameuagiza Wakala wa Vipimo (WMA) kukomesha matumizi ya kipimo cha lumbesa ambacho kimekuwa mwiba mkali kwa wakulima nchini.


Amesema, tatizo la lumbesa limekuwa la muda mrefu na wakulima nchini wamekuwa wakilalamika mara nyingi lakini bado linajirudi.


"Licha ya wakulima kutumia nguvu nyingi bado wanaumizwa kwenye kipimo cha lumbesa hivyo basi wakala mwende mkalifanyie kazi suala hili kama mtu anataka vitunguu kilo 100 basi apate kilo hizo na kifungashio kiwe cha ujazo huo siyo vinginevyo"amesema


Kuhusu ujenzi wa jengo hilo Majaliwa, aliipongeza WMA, kwa kutekeleza maagizo ya serikali ya taasisi zote za umma kuwa na ofisi makao makuu ya nchi.


"Nawapongeza kwa kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwa na jengo makao makuu hapa Dodoma katika ujenzi huu mnapaswa kuzingatia thamani ya fedha.


"Lakini pia naziagiza taasisi nyingine kuhakikisha kuwa wanatekeleza maelekezo haya ili kuipunguzia mzigo serikali wa fedha kwa ajili ya kupanga nyumba za ofisi"amesema 



Akizungumzia, ujenzi wa Mji wa kiserikali Mtumba awamu ya pili amesema umefikia asilimia 73.4 kwa majengo yote 29 ambayo yanajengwa hivi sasa.


“Hadi kufikia Januari mwaka huu ujenzi wa majengo ya mji wa kiserikali awamu ya pili umefikia asilimia 73.4 lakini zipo wizara ambazo ujenzi wa majengo yake umefikia asilimia zaidi ya 90”amesema


Waziri wa Viwanda na Biasha Dk. Ashatu Kijaji, amesema kuhusu sula la matumizi ya lumbesa tayari serikali imeshaunda Tume ambayo inafanyia kazi jambo hilo na itakuja na majabu nama bora ya kulimaliza.


“Hivi sasa ipo tume ambayo inafanyia kazi suala la lumbesa na itakuja na amjibu ili kabala ya mwaka mpya wa fedha kuanza serikali tutatoa maagizo kwa mujibu wa sheria ya fedha kuhusu lumbesa”amesema


Akizungumza kuhusu jengo hilo amesema limefikia asilimia 70.34 na tayari kiasi cha Sh. bilioni 3.25 kati ya bilioni 6.73 zinazohitajika katika kukamilisha mradi huo.


“Mweshimiwa Waziri Mkuu ujenzi huu unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ya taasisi yetu na hadi sasa umeshatekelezwa kwa muda wa miezi 18 na ukimalika utasaidia sana kuondoa tatizo la uhaba wa ofisi na kupunguza gharama za kupanga majengo binafsi”amesema






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI