Na. Matukio Daima Media, Dar
MABONDIA watakaopanda katika msimu wa Saba (7) wa Knockout Ya Mama rasmi kufanya zoezi la Face Off, leo Disemba 30, kuanzia saa 12 jioni, Magomeni Sokoni.
Zoezi hilo linatarajiwa kuwapa mashabiki, wadau wa michezo na wanahabari fursa ya kushuhudia mabondia wakikabiliana ana kwa ana kabla ya mapambano yao, huku likiongeza hamasa kuelekea siku ya pambano hiyo kesho Disemba 31,2025 katika viwanja vya Posta Kijitonyama.
Aidha, Waandaji wa ngumi hizo wamebainisha kuwa, tukio hilo la Face Off itaoneshwa LIVE kupitia: TV3 — Startimes Ch 197 & 131 TV3 Sports — Azam TV Ch 416, Mafia Online TV — Live Stream.
"Mashabiki wote wanakaribishwa kujumuika kushuhudia tukio hili muhimu kabla ya historia kuandikwa ulingoni.
"Burudani ya kufunga mwaka na kufungua mwaka mpya inaanzia December 31 Viwanja vya Posta — Kijitonyama, Kwa Viingilio: Kawaida (Regular) — 10,000/= VIP — 20,000/= VVIP — 50,000/=.
Njoo ushuhudie usiku wa ngumi kali, mashindano ya hadhi ya juu, na historia mpya ikiandikwa ulingoni!" Imeeleza taarifa kwa Umma kutoka waandaaji wa ngumi hizo Mafiaboxing Promotion.






0 Comments