Header Ads Widget

WATOTO ZAIDI YA LAKI MBILI KUPATIWA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA MKOANI KILIMANJARO.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.              

 

WATOTO wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 253289 katika mkoa wa Kilimanjaro wanatarajiwa kupatiwa chanzo ya Surua na Rubella katika kampeni inayotarajiwa kuanza Februari 15 hadi 18 mwaka huu.

 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa, zoezi hilo ni kampeni ya kitaifa huku kauli mbiu yake ni ‘Onesha upendo mpeleke mtoto akachanje’.

 

Babu alisema kuwa, zoezi hilo la chanjo hufanyika kila baada ya  miaka mitatu hadi mitano kwa lengo la kutoa dozi ya nyongeza kwa watoto ili kuwaongezea kinga ya kupambana na ugonjwa wa Surua na Rubella ambapo jumla ya vito 346 vinavyotoa huduma za chanjo vitatumika katika halmashauri zote za mkoa wa Kilimanjaro.

 

“Niwathibitishie kuwa chanjo hizi zinazotolewa ni salama na zimethibitishwa na shirika la Afya ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya na hutolewa bure kwa watoto wenye umri kuanzia miezi 9 hadi chini ya miaka mitano” alisema Babu.

 

Aidha Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Viongozi wa siasa, Serikali, Dini na Jamii katika ngazi zote kuungana kwa pamoja kuhamasisha Jamii, Wazazi na Walezi kuonesha upendo kwa watoto kwa kuwapeleka vituoni wakapate chanjo.

 

Alisema kuwa, athari za ugonjwa wa Surua na Rubella ni kubwa ikiwa ni pamoja na upofu, matatizo ya moyo, matatizo ya ukuaji wa mwili na hata kifo.

 

Mwisho....

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI