Header Ads Widget

UJENZI WA KITUO CHA AFYA URU KUSINI WAKAMILIKA..

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


WANANCHI wa kata ya Uru Kusini jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Patrick Ndakidemi pamoja na Diwani wa kata hiyo kwa jinsi walivopambana kuwaletea kituo cha Afya ambacho kimekamilika. 



Andrew Lyimo alisema kuwa, awali walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hasani kwa jinsi ambapo wanasogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi. 



"Tunampongeza sana Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hasani pamoja na Mbunge wetu Prof. Patrick Ndakidemi na Diwani kwa jinsi ambavyo wanajitolea kututumikia sisi wananchi wa kata ya Uru kusini na kutuletea miradi mbalimbali ya maendeleo" Alisema Lyimo. 



Alisema kuwa, kituo hicho cha Afya pia kinahudumia wananchi wa kata za jirani na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. 


Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI