Header Ads Widget

OTHMAN MASOUD OTHUMANI SASA RASMI KUGOMBEA UENYEKITI ACT WAZALENDO

 


NA MWANDISHI WETU

MATUKIO App, UNGUJA


Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Februari 15, 2024 amechukua Fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Taifa.


Othman amepokea fomu hiyo ambayo imedhaminiwa na kukabidhiwa kwake kutoka kwa Wenyeviti na Makatibu wa ACT-Wazalendo wa Mikoa 27 ya Kichama ya Tanzania Bara na Zanzibar.



Hafla hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Kigoma, Kiiza Mayeye imefanyika katika Ofisi kuu ya Chama hicho, Vuga Mjini Unguja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI