Header Ads Widget

WANAOPISHA UWANJA WA NDEGE KIGOMA WALIA FIDIA KUCHELEWA

Fadhili Mayogela mmoja wa wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye nyumba yake inavunjwa na kulipwa fidia kupisha mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege kigomaNa Fadhili Abdallah,KigomaWAKAZI 360 kutoka kata tatu za manispaa za manispaa ya Kigoma Ujiji wanaopisha maeneo yao kwa ajiili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma wameiomba serikali kuharakisha kulipa fidia ya maeneo kutokana na adha kubwa wanayopata sasa baada ya kuzuiwa kutofanya chochote kwenye maeneo hayo kwa sasa.Wakizungumza na waandishi wa Habari mjini Kigoma wananchi hao walisema kuwa wakati huu wa mvua nyingi wanapata adha kubwa ikiwemo kuanguka kwa nyumba zao lakini maji kuibuka ndani ya nyumba kama chemchem adha ni kubwa kwao ni bora walipwe watafute la kufanya. Mmoja wa wananchi hao, Fadhili Hamisi Mayogela kutoka kata ya Machinjioni Ujiji mjini Kigoma alisema kuwa tangu mwezi Machi mwaka jana walizuiwa kutofanya chochote kwenye nyumba hizo kwa maana watalipwa fidia ndani ya miezi sita lakini hakuna kilichofanyika. Kufuatia hali hiyo mwananchi mwingine Salama Ramadhani Bilali  amemuomba Raisi Samia Suluhu Hassan aingilie kati suala hilo kutokana na sintofahamu inayokumba na kwamba kama serikali haina pesa za kulipa kwa sasa iwaruhusu wafanyie ukarabati nyumba zao na fidia ifanyike upya watakapopata fedha za kulipa.Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye amekiri kuwepo kwa mpango wa fidia kwa wananchi wa kata tatu za manispaa ya Kigoma Ujiji ambao wanapaswa kuondoka maeneo yao kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma. Mkuu huyo wa mkoa amekiri kuchelewa kufanyika kwa malipo hayo ingawa amebainisha kwamba serikali inafanya juhudi kuhakikisha malipo hayo yanafanyika ili malipo ya fidia yasiwe kikwazo kwa utekelezaji wa mradi huo ambao tayari umeshaanza.Baadhi ya nyumba za kata ya kitongoni manispaa ya Kigoma Ujiji ambazo zitavunjwa na kulipwa fidia kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI