Header Ads Widget

DC MBOZI APIGA MAARUFU WATUMIS HI IDARA YA AFYA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA.

Na Ibrahim Yassin, Songwe KAULI za matusi na kejeli zinazotolewa na baadhi ya watoa huduma kwa wago njwa kwenye vituo vya kutolea tiba zime mfanya mkuu wa wilaya ya Mbozi mkoa ni Songwe kuagiza watumishi wa afya kuvaa vitambulisho mda wote wawapo kazini  kwenye vituo vya kazi.Imeelezwa kuwepo kwa dharau, kauli ziaizo na staa kwa wagonjwa zinazof anywa na baadhi ya wauguzi hasa kwa mama wajawazito,wazee na watoto hali iliyomuibua mkuu wa wilaya na kutoa maagizo.Lengo la mkuu wa wilaya ya Mbozi mkoani hapa  Ester Mahawe amepiga marufuku watu mishi wa afya kufanya kazi bila kitam bulisho lengo ni kuwa saidia wagonjwa kuwabaini kwa majina watoa huduma wanaotoa lugha za matusi.Mahawe ametoa agizo hilo jana katika kikao kilicho wakutanisha timu ya usima mizi huduma ya afya, waganga wafawi dhi wa hospitali, vituo vya afya ,zahanati na watumishi wa hospitali lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wilayani humo.Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu huyo wa wilaya  kupokea kero za matusi na kejeli zilizowalenga watoa huduma kwa wagonjwa hususani mama wajawa zito zimemfanya kutoa kauli ya  serikali kumt aka kila mtumishi wa afya kuvaa kitamb ulisho anapokuwa anafanya kazi."Watoa huduma wilayani Mbozi baadhi yenu mmelalamikiwa kutoa lugha mbaya na za karaha kwa wagonjwa hasa wanao kuwa katika hali ya kujifungua acheni tab ia hiyo dawa yenu inachemka," amesema Mahawe.Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wil aya ya Mbozi Alex Mugeta amesema ata hakikisha anasimamia uvaaji wa vitamb ulisho vya kazi kwa watumishi wote ili ku warahisishia wagonjwa kuwatambua watoa huduma wanaowatukana.Mmoja wa wananchi Anastazia Ramadh ani amesema baadhi ya watoa huduma za afya wamekuwa kero Kwa wagonjwa kutokana na lugha chafu na kejeli wanaz okutana nazo hali ambayo husababisha kuogopa kutibiwa hospitali za serikali.Mawazo Mwabeza amesema utaratibu ulioagizwa na mkuu wa wilaya juu ya uva aji wa vitambulisho kwa watumishi wa af ya utatusaidia kubaini majina ya wahudu mu wanaotukana matusi hususani wake zetu wanapokuwa chumba cha kujifung ulia.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI