Header Ads Widget

MAJINA YA MAREHEMU YAZUA SINTOFAHAMU KESI YA MIRATHI NZEGA


NA, MATUKIODAIMA App

MAJINA mawili tofauti yamezua kizungumkuti katika shauri la mirathi ya marehemu Zena Jalakhan ambaye hakuacha mtoto wala mume.


Upande wa pili wa ndugu wamewasilisha pingamizi wakipinga Karim Samji kusimamia mirathi na kutekeleza amri ya Mahakama.


Mapingamizi hayo yenye hoja tatu yaliwasilishwa jana katika Mahakama ya Mwanzo Nzega mbele ya Hakimu Mfawidhi Abunas Sonyo.



Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Sonyo ilimteua Karim kuwa msimamizi wa mirathi ya mali ya marehemu Zena ambayo ni nyumba iliyopo Mtaa wa Ntinginya wilayani Nzega mkoani Tabora yenye namba NTC/NMSH/NTI/81..


Mahakama hiyo pia mbele ya Hakimu Hilda Kibona ilimteua Salma Mohammed kuwa msimamizi wa mirathi ya Zainabu Jalakhan ambayo nyumba iliyopo kwenye mirathi ni hiyo hiyo iliyopo Mtaa wa Ntinginya wilayani Nzega yenye namba NTC/NMSH/NTI/81.


Wiki iliyopita  baada ya Mahakama kufanya Usuluhishi kwa familia, iliamuru  aliyeteuliwa kusimamia mirathi, Karim akusanye mali za marehemu.


Baada ya uamuzi huo, Wakili Edward Malando anayemwakilisha Salma Mohammed aliwasilisha pingamizi kwenye shauri la mirathi ya marehemu Zena Jalakhan ambalo mwombaji ni Karim Kassamali. 


Katika pingamizi hilo Salma amewasilisha hoja tatu, akidai kwamba shauri linalomuhusu marehemu lilikwisha sikilizwa na kutolewa uamuzi katika shauri la mirathi namba 24/2023.


Hoja ya pili mali iliyotajwa katika maombi hayo ilikwishaorodheshwa katika mirathi namba 24/2023 mbele ya Hakimu Hilda Kibona.


Na hoja ya mwisho ni  kwamba shauri hilo lenye viini hivyo lilishasikilizwa na kuamuliwa na mahakama hiyo hivyo aliomba maombi ya mirathi namba 35 ya mwaka jana ya mali ya Zena Jalakhan ambayo mahakama ilimteua Karim kuwa msimamizi yatupiliwe mbali.


Hata hivyo katika nyaraka mbalimbali za nyumba hizo ikiwemo risiti za Kodi ya pango zinasomeka kwa jina la Zena Jalakhan.


Wakili Malando hakuwepo mahakamani kwa sababu alikuwa na dharura hivyo aliomba shauri liahirishwe hadi Februari 16 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mapingamizi.


Awali wakati Mahakama inatoa uamuzi wa kumteua msimamizi wa mirathi Karim hakukuwa na pingamizi kutoka kwa wanafamilia lakini baadaye aliibuka Salma ambaye ni mtoto wa mdogo wa marehemu akafungua shauri akiomba kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi.


Baada ya Mahakama kuona mvutano huo iliamuru pande hizo mbili kuingia kwenye Usuluhishi na baada ya kumalizika iliamuru msimamizi aliyeteuliwa awali kuendelea kusimamia mirathi.


Hakimu Sonyo alisema msimamizi wa mirathi anatakiwa kukusanya mali za marehemu, kuwasilisha orodha ya mali hizo na mgao mahakamani Februari 13 mwaka huu ambapo walifanya hivyo na kukutana na mapingamizi.


Alidai marehemu hakuacha wosia na maelezo hayo yaliungwa mkono na wajukuu, Gullam Siager na Haji Seager hivyo mahakama ikamteua kusimamia mirathi hiyo.


Marehemu aliacha nyumba moja iliyopo mtaa wa Ntinginya wilayani Nzega yenye namba NTC/NMSH/NTI/81.


Wanafamilia katika mirathi hiyo ni wajukuu, Araf Seager, Azaz Seager, Haji Seager, Asha Seager, Gullam Seager, Fatuma Seager, Kasu Seager na Karim Samji ambaye ni mtoto.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI