Na MatukiodaimaApp, Mtwara
Mkaguzi wa Mbegu kutoka Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Salehe Kombo Waziri amewakumbusha wakulima mkoani mtwara kutumia mbegu bora zilizothibitishwa na taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 12, 2024 alisema kuwa wamejipinga kutoa elimu kwa wakulima ili kuweza kujua umuhimu wa kutumia mbegu bora.
“Sisi jukumu letu kubwa ni kusimamia uzalishaji wa mbegu na makampuni yanayojishughulisha na mbegu ambapo tunafanya kaguzi zetu ili kubaini mbegu zilizopitwa na wakati huwa tunatoa agizo la kuzuia zisiuzwe na ziharibiwe”
Wakati wa zoezi la kuharibu mbegu kampuni husika huomba kibali cha kuharibu mbegu zilizopitwa na wakati
”Unajua kitu cha kwanza ni vema kutumia mbegu bora unapoenda kununua hakikisha unaenda kukununua katika maduka ambayo yamesajiliwa na TOSCI ndio jukumu letu kuwasajili pia iwe na taarifa zote muhimu kwenye kifugnashio ikiwemo lini ilipimwa, aina gani, muda wake wa kuisha ni lini iwe na lebo ya ubora” alisema Waziri
kwa upande wake mkaguzi wa mbegu kanda ya kusini Clara Makwinya alisema kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa mkulima hadi mkulima mdogo anatumia mbegu bora zilizopitishwa na taasisi hiyo.
Amesema kuwa ili kuboresha kilimo nchini tumekuwa tukikagua mashamba ya mbegu yanayosajiliwa na TOSCI kila msimu na kuchukua sampuli za mbegu kwa lengo la kupima ubora wake.
Hata hivyo tunapima mbegu maabara na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala na maduka ya kuuzia mbegu.
mbegu bora inalipa na ukitumia lazima kuna kitu utapata ambapo sasa tumeendelea zaidi ambapo wakulima wanaweze kudhibitisha ubora wa mbegu kidigitali” alisema Makwinya.
0 Comments