Header Ads Widget

WANANCHI WAPEWA SOMO KUTHIBITI TEMBO WAVAMIZI WA MASHAMBA NA MAKAZI

 



Na Scolastica Msewa, Saadani.


Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Saadani Simon Aweda amewataka Wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi za taifa kulima mazao ambayo nichukizo kwa Tembo na kufuga nyuki ili kumsaidia kudhibiti wanyama hao kuingia katika makazi na mashamba yao wasifanye uharibifu.


Amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Saadani Chalinze mkoani Pwani kuhusu kujibu malalamiko ya Wananchi wa Maeneo ya Kiwangwa kwamba Kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya tembo kuvamia mashamba na makazi ya Wananchi jambo ambalo ni hatari kwa Wananchi hao.


Ameyataja mazao ambayo tembo hawayapendi sana kuwa ni pamoja na zao la pilipili, zao la alzeti, ufungaji wa nyuki kwa kuweka mizinga ya nyuki kuzunguka maeneo ya mashamba na makazi yao.


"Mizinga ya nyuki kwa kuweka pembezoni ikiwa na nyuki husaidia kufukuza tembo wasiingie kwenye mashamba na makazi ya watu na pia Kuna  mbinu ya kutengeneza tofali za Kuchanganya na pilipili na mavi ya tembo ukichoma moto tofali hizo ndani ya maeneo yako husaidia kufukuza tembo na kudhibiti uharibifu huo unaweza kusababishwa na wanyama poli hao" amesema Aweda.


Aweda amesema Uongozi wa Saadani umekuwa ukitoa elimu kwa Wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ikiwa ni pamoja na kuweka vikosi vya kudumu kwenye maeneo ambayo kumekuwa na matukio ya wanyama poli kuvamia ili watoe msaada wa haraka wanapovamia makazi au mashamba ya watu ili waweze kuwarudisha hifadhini kwa wakati bila kuleta madhara.


Aidha Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Saadani huyo ameomba ushirikiano wa Wananchi na kuwataka kuzingatia elimu walizopewa kwa kulima mazao hayo na kuelekea wapi uvamizi umefanyika na kutoa taarifa kwa wakati ili msaada utolewe haraka.


Amesema Hifadhi za taifa na wanyama waliomo humo ni mali ya Wananchi Bali jukumu la TANAPA ni kulinda ili kuhifadhi raslimali hizo ziendelee kuingizia taifa mapato hivyo Wananchi wanawajibu wa kuhakikisha usalama wa wanyama poli hao wakiwemo tembo.


Aweda pia amesema tembo hawapendi makelele hivyo Wananchi wakiwaona tembo watumie mbinu ya kupiga madebe wakiwa mbali nao husaidia kufukuza tembo mashambani na kwenye makazi ya watu.


Hatahivyo amesema wanatarajia kuongeza askari kwenye baadhi ya maeneo ambayo kuna changamoto kubwa ya wanyama kuvamia ili kuongeza nguvu ya kudhibiti wa wanyama poli haraka.


Awali Mfugaji na mkulima wa Kijiji cha Kiwangwa kitongoji Cha Misani Oliva Rema amelalamikia kuwepo kwa tembo wanaovamia mashamba na makazi ya watu na kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao.

+++++++++

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI