Header Ads Widget

ROCMAX YAWAKUKBUKA MAFUNDI UJENZI, RANGI DODOMA,

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka mafundi Ujenzi na mafundi Rangi ambao wanaendelea kujenga miradi ya serikali iliyopo Dodoma kutoa taarifa za Unyanyasaji wanaofanyiwa na wakandarasi wa miradi hiyo. 


Kauli hiyo ameitoa Dodoma wakati akifunga mafunzo ya mafundi Ujenzi, na mafundi rangi yaliondaliwa na Kampuni ya ROCKMAX INTERNATIONAL LTD ambao ni watengenezaji wa bidhaa ya Extra Power Skimming Putty lengo likiwa ni kuwafanya mafundi hao kuwa na viwango zaidi na kuweza kujiajiri . 


Mkuu huyo amesema Mkoa wa Dodoma unamiradi mingi ya kimkakati na kaguzi za mara kwa mara zimekuwa zikifanyika  na malalamiko mengi kwa mafundi ni pamoja na wakandarasi kutowalipa kwa wakati stahiki zao huku wengine wakilazimika kutoa rushwa ya fedha ili Kupata ajira. 


"Sasa tunakwenda kushughulikia kwa wale wote ambao wamekuwa wakiwaletea vikwazo kutowalipa fedha zenu kwa wakati na wale wanaotaka rushwa kikubwa ninachoomba kwenu ni kunipatia taarifa msikae kimya ili tuweze kulimaliza tatizo, "Amesema 

Aidha Sanyamule amewataka mafundi hao kuacha wizi wa vifaa kwenye miradi jambo litakalowafanya kuaminiwa na kuongeza upatikanaji wa kazi zaidi huku akikisitiza kuacha kutumia lugha za matusi wanapokuwa wanafanya kazi. 


" Muache udokozi wa vifaa sehemu za kazi hiyo itawaondolea sifa na kutoaminiwa kwani hapa Dodoma Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akileta miradi mingi hiyo yote ni kuwapatia Mafundi ajira hivyo nisisitize muwe waadilifu, " Amesema Senyamule


Awali akisoma Risala Mkurugenzi kutoka Kampuni ya ROCKMAX INTERNATIONAL LTD watengenezaji wa bidhaa ya Extra Power Skimming Putty  Hamoud Shabibi amesema mchango wa Mafundi ujenzi ni mkibwa kwa maendeleo ya kiuchumi npamoja maendeleo ya kijamii kwani w amekuwa wakitumia nguvu na maarifa ili kuakisha kazi zao zinaenda vyema. 


" Niukweli usiopingika Mafundi ujenzi ni watu muhimu kwenye maendeleo ya kiuchumi na tunamshukuru Rais Samia kwa kuhakikisha Mafundi wanashiriki katika miradi ya kimkakati inayoendelea hapa Dodoma na sehemu nyingine na Sisi kampuni ya Extra Power Skimming Putty tunaahidi kuwa pamoja na serikali na Mafundi, "Amesema Mkurugenzi hiyo. 

Na kuongeza "Tunahaidi tutakuwa na Mafundi begakwabega na tunaimani umaja huu tumishirikiana na Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) utawezesha kupata kazi kwenye miradi mingi inayoendelea hapa Dodoma, " Amesema


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mafundi Mkoa wa Dodoma Daniel Juma amesema Chama Chao kinamalengo ya kuhakikisha kumuendeleza fundi kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi na kijamii. 


Amesema kutoa elimu juu ya usalama pahala pa kazi na jinsi gani wanaweza kujikinga na bidhaa wanazozitumia ili sisihatarishe maisha yao bila kusahau kuwainganisha Mafundi na mifuko ya uhifadhi ya jamii lengo wakizeeka wapate kiinua mgongo. 


Ameomba Mafundi ujenzi waliopo Dodoma kujiunga na chama ili wapate chombo cha kuwasemea kwani mpaka sasa ni wanachama 63 tu ndio wamejiunga Dodoma..


Pia amewataka Mafundi kuzingatia  ujenzi kwa viwango bora vya majengo ili kuaminika na kupatiwaiaradi mingine inayoendelea Mkoani Dodoma. 


Hata hivyo Mafundi Rangi na Ujenzi takribani 1000 Jijini Dodoma wamepatiwa Mafunzo hayo yenye lengo la kuwapa mbinu za kisasa za ujenzi na matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyostahili katika kukamilisha shughuli zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI