Na Ibrahim Yassin Songwe ,Matukio Daima App Songwe
Wazazi na Walezi Mkoani Songwe wametakiwa kutowachanganya watoto wenye jinsi tofauti katika chumba kimoja ili kuepuka vitendo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa Februari 21, 2024 na Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Mbozi Mkaguzi wa Polisi Saada Salum akitoa elimu ya madha ra ya ukatili wa kijinsia kwa wananchi waliofika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwaajili ya kupatiwa huduma.
"Imebainika kwamba vitendo vya watoto kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi vinaanzia majumbani ambapo watoto wenye jinsi mbili tofauti wnalala chumba kimoja na wakati mwingine hata kitanda kimoja, jambo hilo hupelekea kuanza mahusiano wakiwa wadogo na kuhatarisha mfumo wao wa akili" alisema mkaguzi huyo
Ameeleza kwamba watoto wanapoonza vitendo vya mahusiano ya mapenzi wakiwa wadogo hupelekea kutokuwa na mwamko tena wa masomo na badala ya kujiingiza kwenye vitendo hivyo na watu wenye umri mkubwa ambapo ndio chanzo cha ukatili wa kijinsia.
Aidha amewataka wanaume kutotelekeza watoto wao kwani kufanya hivyo ni chanzo cha kuwa na watoto wa mitaani na ongezeko la watoto kubakwa na kulawitiwa ili wapate mahitaji yao na wakati mwingine hata kusaidia familia.
Hivyo amesema ni jukumu la kila mzazi/mlezi kuhakikisha anatoa huduma bora kwa mtegemezi wake ili kupunguza vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto katika jamii yetu.
0 Comments