Header Ads Widget

MAAFISA UELIMISHAJI UMMA TOENI ELIMU ATHARI YA RUSHWA, MADAWA YA KULEVYA

 

Na Hamida Ramadhani, Matukio Daima App Dodoma.

MAAFISA wanaohusika na uelimishaji umma na mawasiliano wametakiwa  kutoa elimu ya athari ya rushwa na madawa ya kulevya kuanzia shule za msingi, Sekondari hadi Vyuoni ili kulinusuru kundi la watoto wenye miaka kati ya kumi hadi kumi na mbili ambalo kwa siku za hivi karibuni limetajwa kuwa hatarini zaidi kwenye uraibu wa dawa za kulevya.


Kamishina wa kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya Programu ya TAKUKURU rafiki katika tatizo la dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Rushwa huku akibainisha kuwa mafunzo hayo yatasaidia kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya na Rushwa kwani ni vitu vinavyofanana.

Amesema  kupitia muunganiko wao na klabu ambazo tayari wameshanzianzisha mashuleni itasaidia kuwafikia kwa uharaka zaidi watu katika ngazi za mitaa hadi  kwenye Halmashauri kwani wanafunzi wengi wanatokea huko. 


"Matunda ya ushirikiano kati ya TAKUKURU na taasisi ya kupambana dawa za kulevya tayari yameanza kuonekana kwani vitu hivyo vimekuwa vikiisumbua serikali katika kuhakiksha wote wanao husika wanatiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua za kisheria, " Amesema .

Na kuongeza “Nitoe wito kwa wadau kuwa nyenzo pekee ya kuepusha watu kujiingiza kwenye Rushwa na dawa za kulevya ni kutoa elimu hata tukiendelea kukamata kwa namna gani lazima tuhakikishe tunatoa elimu pamoja na kushirikiana na vyombo vya habari ili watusaidie kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja,” Kamishina Lyimo amesema.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Neema Mwakalile amesema kilichotokea kwenye mafunzo hayo kinadhihirisha ushirikiano  uliopo kati ya TAKUKURU na Mamlaka ya Kupambana na dawa za Kulevya ni mkubwa kwani vitu hivyo vinafanana na mapambano yanapaswa kuimarishwa zaidi.


Ameeleza kuwa washiriki wamejifunza juu ya tatizo la dawa za kulevya, sababu za matumizi ya dawa hizo pamoja na kutambua dawa tiba ambapo vijana wengi wameonekana kujiingizia kwa kiasi kikubwa katika janga hilo huku akiongeza kuwa elimu waliyo wapatia washiriki katika mkutano huo itaenda kuumarisha zaidi mapambano na hatimaye kufikia hazma ya Serikali.

“Washiriki walipitishwa kwenye mkakati wa kupambana na Rushwa ili kuelewa zaidi na namna ya kwenda kuelimisha wanafunzi pia mafunzo haya yatasaidia jamii kuichukia Rushwa na kuepukana na  Dawa za kulevya,”amesema.


Pia ameongeza kuwa katika mambo mengi waliyowafundisha wataenda kutoa elimu hasa kwa wanafunzi kwani swala hilo limekuwa mtambuka. 


 “Ni lazima kuanza kuwajenga wanafunzi wa shule msingi na sekondari kwani wao ndio watakuwa msingi mzuri kwenda kupinga na kukataa dawa za kulevya pia  Rushwa na dawa za kulevya vina madhara makubwa kwenye nyanja zote elimu na uchumi,”ameongeza.


Taasisi ya kupambana na Rushwa na TAKUKURU waliingia makubaliano 20/5 2023 kwaajili ya kutoa elimu kuhusu rushwa na dawa za kulevya.

Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS