Na Mwandishi wetu, Matukiodaima App, Mtwara
Maafisa ugani zaidi ya 31 kutoka Wilaya ya Mtwara wapatiwa mafunzo ya zao la ufuta katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Naliendele mafunzo ambayo yataboresha zao hilo ili wakulima walime kwa tija na kuvuna mazao mengi zaidi.
Akizungumza na maafisa ugani hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Abeid Kafunda amewataka kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo ili kuhakikisha kuwa wakulima wanaoongeza mavuno na kukua kiuchumi.
Amesema ni muhimu wakulima kukumbushhwa upandaji wa zao la Ufuta, nafasi kati ya mche na mche, mstari kwa mstari pamoja na kudhibiti magonjwa na vijidudu visumbuu vya mmea huo.
“Sawa tumetoa mafunzo nawasihi yakawe mfamo mzuri yakwe chachu ya kuboresha zao la ufuta katika halmashauri yetu ya Mtwara na tukumbuke kuwa ufuta sio kama mahindi ambayo unaweza kulima sehemu moja kila mwaka ila ufuta unalima kwa awamu yaani ukilima mwaka huu mwakani unalima kitu kingine ili kuepuka vijidudu visumbufu” amesema Kafunda.
“Lakini nimefurahi kusikia kuwa somo la leo lilihusiana na zao moja tu la ufuta ambalo ndio zao ninalolipenda na niliwahi kuwa na wazo la kulima ufuta ambapo nilielezewa changamoto zake na nimefika na nimejifunza kuhusu ufuta nimeelewa nitaendelea kujifunza zaidi” amesema Kafunda
Nae Mkurugenzi wa TARI kituo cha Naliendele Dkt. Furtunus Kapinga amesema kuwa mafunzo hayo ni chachu na pia yatongeza uahamu kwa maafisa hao juu ya zao la ufuta.
Amesema kuwa upo umuhimu wa watalaamu hao kukumbushana umuhimu wa zao la ufuta na kuifahamu agrononimia ya zao hilo.
Nae Mratibu wa Programu ya Utafiti wa Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda amewasisitiza maafisa hao kutoa elimu stahiki kwa wakulima wao ili waweze kulima kwa tija.
“Tumefanya mafunzo rejea kwa watalaamu wa kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya mtwara tumewafundsisha ili waweze kuongeza uzalishaji lakini pia kuongeza tija ambapo tumewafundisha agronomia ya zao lenyewe la ufuta pia tumesisitiza namna bora ya kudhibiti wadudu na magugu”
"Pia namna ya kuhahakikisha kuwa zoa linakuwa na afya kwa maana ya kuangalia rutuba ya udongo pale inapohitajika” amesema Nzunda
Nae Afisa Kilimo Kata ya Tangazo Thomas Mpemba amesema kuwa mafunzo hayo yamewapika na kuwaongezea uelewa zaidi.
“Yaani hapa tumeongezewa uelewa katika teknolojia ya kilimo ambapo tumeongeza uelewa kwenye zao la ufuta unajua kilimo kina mabadiliko ya aina mbalimbali ambapo ikiwemo namna bora ya kudhibiti magonjwa na visumbusu katika zao hilo” amesema Mpema
Afisa Kilimo Kata ya Msangamkuu Maonyesho Said amesema kuwa kutokana na hali ya mazingira wakulima wanapaswa wakubaliane na mabadiliko ya tabia nchi.
0 Comments