Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP Moshi
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro (2005-2010) Fuya Kimbita (CCM)ni miongoni mwa wabunge waliofanya kazi kwa ukaribu na hayati Edward Lowassa aliyehudumu pia kama waziri mkuu katika serikali ya awamu ya nne.
Kwa mujibu wa Kimbita ni kuwa hayati Lowassa alikuwa ni kiongozi wa kipekee mwenye maono uthubutu na utayari wake katika kuwahudumia watanzania.
'Uongozi ni alama na yeye kama kiongozi kaacha alama mfano kaangalie shule za sekondari za kata ambazo ziliasisiwa na yeye kila kata nchini ikawa na sekondari yake nyingine hadi mbili hizi ni jitihada zake'anasema
'Watu hawakujua malengo yake lakini yeye hakukatishwa tamaa Kwa kile alichokuwa anakiamini lakini leo hii watanzania wanaona manufaa yake'anasema
Kimbita anasema kuwa katika kipindi cha uongozi wake pia kulitokea baa la njaa na kuwa aliyekuwa waziri mkuu hayati Lowassa alihakikisha kila kaya yenye uhitaji wa chakula walipatiwa kwa wakati.
'Alikuwa anakupigia simu usiku kwamba mbona jimboni nimesikia kuna njaa haya nenda pale ofisi za maafa kachukue chakula uwapelekee mara moja'anasema
Anasema alama nyingine ni pamoja na kutoa maji katika ziwa Victoria jambo ambalo wanachama wengine waligoma kwa kisingizio kuwa anakiuka mkataba lakini hakusikiliza wala kutetereka na hatimaye maji yakatoka kama ilivyokuwa dira yake.
'Nitamkumbuka kwa kweli na tuzidi kumuombea maana kwanza aliheshimu kila mtu mkubwa na mdogo na uzuri alikuwa ni msikivu kwa wote'Anasema
Anasema endapo hayati Lowassa angekuwa ni mtu wa visasi basi angewaumiza walio wengi kwani uwezo huo alikuwa nao na hali ya kiuchumi pia alikuwa nao mzuri lakini hakufanya hivyo.
'Angeweza kutumia fedha au madaraka yake lakini hakuwa mtu wa visasi hata kidogo licha ya watu wengine kumdhihaki na kumtukana hakuonyesha kujibu mapigo'anasema
0 Comments